Watu wengi tunatumia kompyuta kutazama filamu na sinema (movies) mbalimbali, lakini kuna baadhi ya filamu huwa hazionyeshi manukuu (subtitles) hivyo tunapata changamoto sana ya kuweka manukuu (subtitle) na unatamani kuona manukuu (subtitles) ili kuelewa nini wanachokiongea kwenye filamu kwa kusoma hayo manukuu (subtitles).
Kuna programu nyingi za kuangalizia hizo filamu na sinema, moja ya programu maarufu ni VLC (VideoLAN), hii programu inakuwezesha kupakua (download) na kuweka manukuu (subtitles) ya filamu na sinema mbalimbali.
Namna ya kuweka manukuu (subtitles) kwenye filamu (movies)
Fungua filamu yako kwa kutumia programu ya vlc na kama haina manukuu (subtittles), unachotakiwa kufanya, nenda pale juu kwenye menyu (menu) bofya sehemu pameandikwa “View” kwenye machaguo utashuka chini kwenye sehemu imeandikwa “VLsub” bofya hapo itakupeleka kwenye jedwali la machaguo, utaona sehemu imeandikwa “Title” weka jina la filamu/movie uliyofungua ambayo unataka kuona manukuu (subtitles) yake, ukishaweka jina la filamu bofya sehemu ya “Search by Name” utaona majina mbalimbali ya filamu, chagua jina linaloendana na filamu kisha bofya kwenye “Download selection” hapo utaona manukuu (subtitles) zinaonekana kwenye filamu/movie yako.
Kuna baadhi ya filamu zinakuja na manukuu (subtitles) kwenye folda/folder lake, ili kuziweka subtitle kwenye filamu/movie yako ukiwa umefungulia kwenye programu ya vlc, angalia kwenye menyu/menu utaona imeandikwa “Subtitle” bofya hapo kisha bofya chaguo la “Add subtitle file” utachagua file la subtitle/manukuu kutoka kwenye folda la filamu/video hiyo. hapo tayari utaona subtitle/manukuu yakionekana kwenye filamu.
Kuna wakati unaweza kuweka manukuu/subtitle kwenye filamu yako lakini zikawa zinapishana, mfano mtu anaweza kuongea huku manukuu/subtitle zikichelewa kuonekana au zinaweza kuwa mbele kabla ya mtu hajaongea au kitendo flani kufanyika, unaweza kurekisha hiyo changamoto kwa kutumia kibodi/keyboard, tumia herufi G na H, hizi herufi zinasaidia kurekebisha hilo tatizo.
Kama manukuu(subtitle) yanachelewa yaani tukio limeshafanyika ndiyo inaonesha subtitle, unatakiwa kubofya herufi G mpaka ziendane, na kama manukuu (subtitle) yanawahi basi itabidi ubofye herufi H ili subtitle ziendane na filamu/movie.
No Comment! Be the first one.