Instagram kwa sasa ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana na yenye wafuasi wengi wengi sana duniani.
Mitandao kama hii (Instagram) huwa inawafanya watu kuwa katribu na kurahisisha mawasaliano kwa njia ya maandishi, sauti au video.
Kumbuka kwa haraka haraka ilikua video moja ikipandishwa katika mitandao hii huwa inapoteza ubora —hii inamaanisha mara nyingi inavyopandishwa na kushushwa basi ubora wake unapotea.
Njii hii ikiitumia itafanya video yako inayopanda katika mtandao wa instagram kuwa na ubora ule ule
Ingia katika ukura wako wa instagram na kisha nenda katika eneo la vidoti vitatu (menu) upande wa juu kulia
Ingia katika eneo la “Settings and Privacy.”
Shuka chini mpaka eneo la “Data Usage and Media Quality”
Hapo inabidi ukubali/uruhusu eneo lililoandikwa “Upload at Highest Quality”
Ukishafanikisha hilo hapo utakua umeshaweza kuwezesha jambo hili na hapa hata ukipandisha faili ambalo lina ukubwa sana litafanikiwa hata kama litachukua muda sana.
Ni wazi kuwa mitandao mingi sana ya kijamii kwa siku hizi inapambana kuhakikisha kuwa inakua na ubora ule ule wa picha au vdeo kipindi zikirushwa, tumeshaona hata kwa WhatsApp —– Soma zaidi >>HAPA<< na >>HAPA<<.
Mitandao ya kijamii huwa inakua na unjanja ujanja ambao ukiutumia ndani yake utaweza furahia zaidi mitandao hiyo kuliko mwanzo, hilo liko wazi sio?
Niandikie hapo chini katika eneo la comment je ulikua unaifahamu njia hii? Ningependa kusikia kutoka kwako
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.