Kujua umefanya nini leo mwaka jana inaweza ikawa ni gumzo kwako sio?. lakini kwa kutumia App ya TimeHop hilo linawezekana. Ukiachana na mambo ya #TBT (throwback thursday) katika Instagram kuna mengi unaweza kugundua uliyofanya katika mitandao yako ya kijamii
Sio lazima uwe mpotezaji wa kumbukumbu kutumia App hii, kumbuka unaweza ukawa ulifanya mambo fulani hivi na kumbukumbu yake ikakuletea kicheko katika siku yako. kwa mfano mimi nikiona Post zangu za facebook za mwaka juzi lazima nicheke, sijui wewe?
Maisha yanabadilika sana siku moja utakuwa unawanunulia watoto wako midoli, baada ya kumaliza utashangaa wanawanunilia watoto wao midoli, kumbukumbu ni muhimu sana. lakini kadri umri unavyozidi kwenda hata uwezo wetu wa kumbukumbu unapungua lakini kama una App spesheli inakuwa rahisi kwako kujua nini ulifanya wakati uliopita (mwaka Jana)

Kumbuka pia teknolojia imefanya mambo yote haya kuwa marahisi, ili kubaki na kumbukumbu unaweza chukua simu yako na kuanza kupiga picha au hata kuchukua video na kisha kutuma katika mitandao yako ya kijamii. baada ya kuzitupia katika mitandao hiyo ya kijamii ni mara ngapi unachukuaga mda wako na kuanza kuziangalia tena? …pengine ni mara moja moja au haufanyagi hivyo kabisa sio?
Kuna App inaitwa Timehop, kazi yake kubwa ni kukukumbusha kitu gani ulifanya mwaka jana kupitia mitandao yako ya kijamii, hapa App inaangalia picha, video na hata post za kawaida na kukumbusha.
Inachukua vitu facebook, instagram na mitandao mingine ya kijamii ambavyo ulivypost mwaka jana na kuvionyesha katika App hii kama kumbukumbu.
Timehop ina kuwezesha kuangalia picha hizo na pia hata kuzituma katika mitandao ya kujamii (kawa ulichokuwa unakifanya mwaka jana si cha ajabu)
No Comment! Be the first one.