Kampuni ya Yahoo imefanikiwa kutengeneza teknolojia mpya inayotambulika kama ‘Bodyprint’ kutambua sehemu/viungo mbalimbali vya mwili wa mmiliki na kuondoa ‘lock’ yake. Ebu fikiria simu iweze kuji ‘unlock’ pale ngumi, sikio au ata kidole chako kikiwa karibu.
Kwa sasa hivi kuna njia mbalimbali za kuondoa ‘lock’ ya simu kama vile kwa kutumia namba, yaani ‘code’, au kutumia michoro na simu za kisasa zaidi zinakuwa na teknolojia ya kufungua kwa kutambua alama za vidole, yaani ‘Fingerprint sensor’.
Inasemekana utumiaji wa teknolojia ya Fingerprint sensor ni ghali sana na inafanya simu zenye teknolojia hii ya alama za vidole kuwa bei ghari sana, lakini teknolojia hii itakuwa na unafuu mkubwa kwani itakuwa inatumia kioo cha simu janja kutambua viungo hivyo vya mtumiaji.
Yahoo wameitambulisha teknolojia hiyo katika kongamano la masuala ya teknolojia za kompyuta huko nchini Korea kusini katika jiji la Seoul. Zoezi zima la simu kuji’unlock’ litachukua chini ya sekunde moja baada ya wewe kuweka simu yako kwenye umbo hilo la mwili. yaani iwe ni sikio, pua au sehemu ya mwili nyingine.
Pia katika mipangilio yako, (settings) utaweza kuweka zaidi ya kiungo kimoja na pia kama simu hiyo mnatumia watu wawili au zaidi basi mnaweza kuweka rekodi ya viungo vyenu wote na hivyo yeyote kati yenu kuweza kuifungua.
Yahoo bado hawajasema itachukua muda gani wao kuanza kuwauzia teknolojia hii watengenezaji simu ila inategemewa kuanza kutumia muda si mrefu.
Habar yk bro cm yang ina tatizo ukisoge mafaili amin page yani ina ckika sauti ya mtu ikisema page one page two etc nim
e restore sim bd haitak msaada tafadhal cm yenyew ni Samsung galaxy s3 mini