Katika habari hii ya kufikiria leo, TeknoKona inataka kuongelea juu ya makampuni ambayo yana mabilioni na mbabilioni (dola) ya hela nyuma yake ambayo yanaziendesha kampuni hizi. Sasa umeshawaji kufikiria dunia itakuwaje kama kampuni za Apple, Google na Facebook zikifa?
Sawa tunajua kama makampuni haya ni makubwa sana na kama yakifa ghafla bila shaka watu wengi sana watapoteza pesa nyingi. Lakini kabla ya kusema mengi ngoja kwanza tuweke mpaka wa kutuongoza katika kudadavua hili
Fikiria Kama: Hakuna taarifa yeyote kutoka kwa kampuni husuka wala mkakati wa kulifufua kampuni
Sasa Tuanze Kujua Nini Kitatokea Kwa Kampuni Moja Moja
1. Watu wataanza kupiga simu kwa ndugu, jamaa na marafiki zaidi (kuliko Facebook ilivyokuwa hai)
2. Watu wataanza kuonana sana kwani kuona rafiki yako ka ‘post’ kitu gani kila siku kinachangia kutoonana mara kwa mara.
3. Uzalishaji utaongezeka kwani watu wengi watakuwa na muda wa kutosha katika kazi zao
4. Makampuni yatasevu mamilioni ya pesa kwa ajili ya utangazaji katika mtandao wa kijamii wa Facebook
5. Tovuti nyingi sana (hasa za burudani) zitakosa watu wa kufuatilia habari zao na baadhi watafunga kabisa tovuti hizo (facebook ni njia kubwa ya kuwapelekwa watu katika tovuti husika kwa kutumia link mbalimbali)
6. Wafanyakazi wengi wa Facebook watapoteza kazi zao
7. Watumiaji wengi sana wa Facebook watakimbilia Twitter na mamilioni ya akaunti yatafunguliwa ili kufuatilia habari juu ya kifo cha Facebook. Pengine labda tovuti ya Twitter inaweza ikapata matatizo ya kiufundi (crash) kwa kuwa na watu wengi sana wanaoingia katika mtandao huo kwa mkupuo.
GOOGLE
1. Makampuni mengi yatapoteza mamilioni ya pesa na mengine kufilisika kabisa
2. Watu wengi watapoteza kazi zao hasa wale wataalamu wa mambo ya SEO. Ukosefu wa ajira utaongezeka kwa kiasi kikubwa
3. Uchumi utaathirika
4. Ubunifu utapata pengo kwani ‘project’ kibao kutoka Google zinazojulikana kama ‘Google X’ zitakufa hii ikiwemo na magari yanayojiendesha yenyewe.
5. Tovuti kama Facebook zitafurika kwani zinaweza zikawa ndio vituo vikuu vya habari tofauti tofauti.
6. Upinzani mkubwa sana utatokea kwa makampuni mengi makubwa yenye tovuti kama vile Facebook na Twitter katika kutaka kuzipa pengo la Google hasa katia umaarufu wake wa kutafuta (search) vitu mbalimbali.
APPLE
1. Maelfu ya App yatapotea na makampuni au watu wanaomiliki App katika AppStore watapata hasara.
2. Maelfu ya wanahisa watapoteza pesa nyingi baada ya umiliki wao kupotea katika kampuni hilo.
3. Mamilioni ya simu duniani yatabaki kama makopo tuu (hazitatumika tuu)
4. Wanotengeneza pesa kupitia iTunes (mfano wasanii) na Mac Tools watapoteza pesa nyingi na watatoka katika biashara.
5. Mamilioni ya simu za Android yatanunuliwa kwa siku moja na kuzifanya kampuni za simu za Android kuingiza mabilioni katika kipindi cha wiki chache tuu.
6. Wauzaji wa simu zenye bei za chini katika soko watauza simu nyingi sana kwani watu watataka kuwa na simu mbadala kwa haraka ili kuendelea na mawasiliano
7. Foxconn, kampuni ambalo lina kitengo kinachozalisha simu za iPhone litafunga kitengo hicho (lakini cha kuzalisha simu za iPhone tuu)
8. Matumizi ya nishati ya mafuta itaongeza. Watu watatembea sana kwenda kuona marafiki, ndugu na jamaa zao.
Kwa haraka haraka kwa mfano kampuni la Facebook likifa maisha ya watu wengi ambao walikuwa wanatumia mtandao huo na wana tabia ya kuiga marafiki zao kwa mfano wamevaa nini. Tabia zao kwa ujumla zitabadilika na wataanza kuishi maisha yao kwa kiasi flani. Kwa kifupi watu watakuwa na furaha zaidi kwani hawataweza jifananisha na wenzao na pia hata ‘mood’ ya watu itabadilika kwani watakuwa hawasomi mambo mengi sana ambapo walikuwa wanafanya wakiwa katika mtandao huo.
Kama kampuni la Google likifa kutakuwa na tikisiko kubwa katika uchumi. Hili linaweza hata kumpelekea mmiliki wa Facebook kuwa baba wa Intaneti
Kifo cha Apple pia kitaathiri vikubwa katika uchumi na pia hata katika soko la hisa duniani hata kwa wawekezaji.Kampuni la Apple limesaidia makampuni mengi sana kutengeneza pesa kama vile Foxconn, makampuni yenye App, wasanii na wengine wengi. Android ndio itakuwa mfalme katika Os za simu janja.