Tayari kampuni ya Google ipo katika utafiti na tayari ishatengeneza mifano ya simu ambazo utakuwa unanunua vipande (parts) na kuunganisha. Yaani hakutakuwa na mauzo ya simu nzima bali utakuwa una’upgrade kwa kununua na kupachika kifaa husika. Na sasa Acer wamekuja na mfumo huo huo na inaonekana muda si mrefu watakuwa ndio wa kwanza kabisa kutengeneza na kuuza kompyuta za teknolojia hii.
Uzuri wa teknolojia hizi ni kwamba tegemea kuweza kununua na kuuza vipisi (parts) unazobadilisha kwa urahisi kwa wengine kwani lengo kuu ni kuhakikisha vifaa hivyo vitaweza kuingiliana kwa urahisi.

Tunamaanisha nini hasa tunaposema ununua vipande na unaunganisha?
Mwanza kabisa utanunua kompyuta hii kiuzima wake ikiwa imeunganisha na sehemu (parts) zote muhimu. Yaani kutakuwa na kipande cha CPU, cha chaji, graphic card, diski (Hard disk), na kipisi cha masuala ya sauti.
Wengi wanategemea teknolojia ya namna hii kutumika kwenye simu janja na kompyuta kutashusha gharama na ulazima wa kutumia pesa nyingi kununua kifaa chenye teknolojia ya kisasa zaidi. Mara nyingi watu wanajikuta wakitumia pesa nyingi kununua simu mpya kisa tuu ya maboresho machache katika simu hizo, kama kungekuwa na uwezo wa kununua na kupachika bila ufundi wowote kitu hicho kipya basi wengi wangeweza kuokoa pesa nyingi sana.

Acer wanaita vipande hivyo vinavyotumika kujenga kompyuta yako ‘Blocks’, yaani matofali. Na zitatambulika kama Acer Revo.
Acer wamesema muda wowote hivi karibuni wataanza kuuza kompyuta za teknolojia hii na hivyo watu wakae tayari kupata uhuru huu wa kipekee wa kuweza kufanya maboresho ya kompyuta zao kirahisi bila kununua kipya kila mwaka.

Mradi wa Google wa kutengeneza simu zinazofuata teknolojia hii unafahamika kwa jina la Project Ara na wanyewe Google wamesema simu hizo zitegemewe kuingia sokoni kuanzia mwaka 2016.
Uzuri wa teknolojia hizi ni kwamba tegemea kuweza kununua na kuuza vipisi (parts) unazobadilisha kwa urahisi kwa wengine kwani lengo kuu ni kuhakikisha vifaa hivyo vitaweza kuingiliana kwa urahisi.

One Comment