Baada ya mabadiliko makubwa kufanyika kwa kampuni ya Google, hii ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa kampuni mama itambulikayo kwa jina la ALPHABET Google waamua kufanya mabadiliko katika logo yao.
Logo mpya yenye muonekano nyororo zaidi wamedai ni nzuri na bora zaidi ata kwenye vifaa kama vile simu, ‘eti’ inafunguka haraka zaidi bila kutumia data nyingi.
Ingawa kwa wengine wanaweza kuona ni mabadiliko machache tuu kwa logo ya kampuni hiyo kiuhalisia ni kwamba kuna mabadiliko mengi ya kiundani zaidi yanaendelea katika kampuni hiyo. Na tunaamini mabadiliko haya ya logo ni moja kati ya mabadiliko mengi yanayoendelea katika kampuni hiyo sambamba na uwepo wa kampuni mpya ya ALPHABET.
Je kati ya logo hii mpya na ile ya zamani ni ipi umeikubali zaidi?
No Comment! Be the first one.