Kwa wengi wetu tutakapowaza kununua kompyuta mara moja tunawaza HP, Samsung au Dell, na mara chache Acer, ila je unajua Lenovo namba mbili duniani kwa mauzo ya kompyuta, tena ndani ya wiki chache zijazo kampuni hii inatemewa kushika namba moja!
Lenovo ikifanikiwa itakuwa ndiyo kwa mara ya kwanza kwa kampuni ya Kichina kushika namba moja katika vifaa cya elektroniki, na haishangazi kwani takribani nusu ya mauzo ya kompyuta za Lenovo yanafanyika nchini Uchina.
Takwimu za soko zilizotoka zinazoelezea hali ya soko la kompyuta, zinaonesha bado Hewlett-Packard (HP), bado ndiyo kampuni kubwa duniani katika uuzaji wa komyuta, ikiwa mbele ya kampuni zingine lakini ikiwa inafuatiwa kwa mwendo kasi wa Lenovo.
Makampuni ya kusoma masoko ya Gartner na IDC, yote mawili siku ya leo yalitoa makadirio yao ya soko. Ingawa wao hupima soko tofauti, wote wawili wameonyesha pengo kati ya HP na Lenovo kuzidi kuwa dogo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Kwa ujumla, Gartner imesema, watu binafsi na makampuni yalinunua kompyuta 87,470,000 katika kipindi cha miezi ya nne hadi sita, ambazo ni sawa na kuporomoka kutoka 87,600,000 katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita. HP imewazidi wachuuzi wengine wote, kwa kuuza mashine 13,040,000 na kuchukua asilimia 14.9 ya sehemu ya soko la duniani kote. Lenovo, kulingana na makadirio ya Gartner, ilipitwa kidogo tuu, iliuza mashine 12,820,000, ambayo ni jumla ya asilimia 14.7 ya soko, na mauzo haya yamevunja rekodi kwa ukuaji wa takribani 15 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
No Comment! Be the first one.