Nothing ni kampuni ya simu na vifaa vya kielektroniki, miezi kadhaa iliyopita kampuni ilitambulisha simu mpya katika soko ambayo iliwavutia wengi.
Kuanzia kauchiwa kwa simu ya kwanza kabisa ya Nothing mpaka sasa ni miezi kadhaa imepita na watu na wadau mbalimbali walikua wanajiuliza sana juu ya ujio mwingine wa kampuni na kifaa kingine.

Pengine kwa sasa jibu limepatikana baada ya kampuni kutangaza kifaa kingine ambacho kitakua sio simu bali ni kafaa kinachotumika katika simu na kwa baadhi ya vifaa vingine.
Sasa inakuja na spika za masikio zisizokua na waya zinazokwenda kwa jina la Ear Stick, spika hizi zitatangazwa na kampuni hiyo rasmi mwezi oktoba tarehe 26 mwaka huu.
Kama simu ya nothing hasa hasa katika jumba lake vilivotushangaza pengine tutegemee mpaka katika spika hizi kutakua na mambo kadha wa kadha ya kushangaza.
Utambulisho huo utafanyika kwa njia ya mtandao kama wengi wanavyofanya siku hizi. Tukio zima litaruka mubashara kupitia katika tovuti ya kampuni hiyo.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi yenye dodoso kuhusiana na kifaa hicho jinsi kilivyo kwa wazi wazi hivyo basi hatuna budi kusubiria siku ya utambulisho
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Je unadhani spika hizo zitateka watu kama vile katika simu (Nothing)?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.