Kutoka kwenye soda hadi kwenye simu…!!! Kuna uhusiano wowote kati ya hivi vitu viwili? Sidhani, lakini kampuni ya Pepsi inafikiri kuna uhusiano. Pepsi ipo katika hatua za mishoni kuweza kuingiza simu inayotegemewa kuitwa Pepsi P1 huko nchini Uchina.
China tayari inaupatikanaji wa simu nyingi sana za bei rahisi zinazotumia Android na Pepsi wameona nao wana nafasi ya kuingiza ya kwao.
‘Nia kuu si kuingia moja kwa moja kwenye biashara ya utengenezaji simu’
Inaonekana wanachofanya ni kuleta simu hii kama sehemu ya vitu vya kuzidi kusambaza ‘brand’ yao ya Pepsi. Kumbuka makampuni kama haya huwa yanauza pia kwa uchache vitu kama vile nguo, mabegi n.k vinavyokuja na logo yao, yaani Pepsi. Na hivyo jambo hili linachukuliwa kama sehemu ya kukamalisha hilo.
Vyanzo mbalimbali vya habari zinazohusu Android vina uhakika juu ya ujio wa simu hiyo kwa asilimia 100% huku ikitegemewa wenyewe Pepsi kutangaza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.
‘Ubunifu na utengenezaji wa simu hiyo unasimamiwa na kampuni ya utengenezaji simu ambayo bado haijajulikana’
Simu hiyo inayotegemewa kuuzwa kwenye bei isiyozidi dola 200 za kimarekani, yaani kwenye laki 4 hivi ina sifa zifuatazo;
- Kioo cha inchi 5.5 (kiwango cha 1080p – HD)
- GB 2 za RAM
- Diski ujazo – GB 13
- Prosesa 1.7GHz
- Betri – 3,000 mAh
- Kamera ya Megapixel 13
Ina ubora mzuri tuu kwa simu ya bei ndogo ila inasemekana kwa nchini China ukipakua vizuri utakutana na ata zenye ubora mkubwa zaidi kwa bei hiyo.
Wengi wanategemea kampuni hiyo kuweza kuuza simu hiyo kwa wapenzi wa kinywaji hicho, je itauzika kwa wingi? Inawezekana ila hakuna uhakika sana, muda utatuambia. Je unamtazamo gani juu ya uamuzi huu? 🙂 Tungependa kusikia kutoka kwako.
Vyanzo; TheVerge, DigitalTimes, Fortune.com
No Comment! Be the first one.