Mmiliki na muanzishi wa kampuni ya IT inayojihusisha na usalama ya Kaspersky Bw. Eugene, amesema katika mkutano wa kiusalama wa AusCERT kuwa Windows ndio programu endeshaji bora kulinganisha na iOS, OS X, na hata Android huko nchini Australia.
Mtaalamu huyo wa mambo ya kiusalama wa kompyuta na simu pia amesema kuwa Windows wameonyesha ubora wa hali ya juu kwani wanajitahidi katika kuboresha usalama wa programu endeshaji (OS) yao.
Microsoft wamekuwa wakifanya jitihada za nguvu juu ya kuangalia ni namna gani wanaweza kuzuia mashambulizi mengi na kuboresha ulinzi wa watumiaji wa Os zake hasa katika hii inayokuja ya Windows 10. Eugene na kampuni lake la kiusalama anachambua zaidi ya 300,000 ya ‘Malwere’ kwa siku, Kampuni limekuwa likiboresha njia ya kisasa ya kujikinga na vitisho ambavyo vinaweza vika athiri kompyuta kwa dunia.
Kampuni imekua ikikusanya taarifa kwa watu milioni 400 ambao ni watumiaji wa kudumu wa kaspersky kuhusiana na sampo za malware na virusi vya aina mbalimbali ili kuona ni OS (operating system) gani ambazo ni dhaifu na ni rahisi kwa watu ku ‘hack’
Benki za kwenye simu zimejulikana kwa kiasi kikubwa cha matukio ya wizi kutokana na watu wengi kuhamia kwenye simu (e-mail na mitandao ya kijamii) katika kufanya miamala yao ya kila siku. Kaspersky wamekuwa wakitoa suluhisho la namna yake —”disconnect from the Internet”— yaani jitoe katika intaneti na hii ikiwa na kinga kwa vifaa vyote
Bwana Eugene pia alisema pia alisema kuwa hana simu janja na pia amekuwa akitumia akitumia sonny ericsson ya kizamani kwa ajili ya mawasiliano.
Kaspersky walisema kuwa siku hizi Antivirisi sio kama zamani jinsi zilivyokuwa zinafanya kazi ya kuzui virusi tuu bali kuna mambo mengi ndani yake siku hizi kama vile uhalifu wa kimtandao, hujuma, upelelezi na kadhalika
Alisema hata kama ni vigumu sana kuzindua ‘malwere’ katika system ya iPhone kwa sababu OS yake imefungwa kwa watu wa nje wa masula ya programing. Kila System ina mapungufu yake na hiyo inaifanya iPhone kuwa na mapungufu makubwa sana katika simu janja. Kitu kibaya kinachoweza tokea ni kama mamilioni ya iPhone yata vamiwa kiusalama, basi tiba haitapatikana haraka kwa kampuni la Apple haliruhusu wataalamu wa nje wa ‘programming’ katika system zao hiyo itapelekea makampuni mengi ya kutengeneza Antivairasi kushindwa kufanya kazi.
Kuhusu Android, Kaspersky wamesema kuwa kutokana na kwamba ni maarufu na ni ‘system’ ambayo iko wazi itakuwa ni rahisi sana kutatua mshambulizi. Kwa mfano hebu fikiria Android imepatwa na majanga (mamia ya simu) itakua ni rahisi kupatia tiba tatizo hilo kwa Android ipo wazi karibia kwa kila mtu. Watengenezaji wa antivairasi hawatapata shida katika kutengeneza kinga.
Cha kufurahisha ni kwamba Kaspersky wemeitaja Os ya Windows kuwa ni Os (Katika simu) kuwa ni ile ambayo iko safi kabisa. Na hii ni kwa sababu njia ya usalama katika simu unaotolewa na Microsoft ni ule wa hali ya juu kama ule unaotolewa na Apple.