Mfumo endeshi wa Android Oreo bado ungali haujaenea katika simu nyingi sana lakini tayari katikati ya mwezi huu kunakaribia kutolewa kwa toleo jipya la majaribio la Android P.
Toleo la majaribio litadumu mpaka pale toleo rasmi litakapozinduliwa likiwa na jina rasmi litakalotambulika badala ya Herufi P.
Kwanini Android P? Kwa sababu Google ambao ndio wazalishaji wa Mfumo wa Android wamekuwa na utaratibu wa kutoa majina yao kwa utaratibu wa herufi zenye kufuatana na kutumia majina ya pipi, peremende au kitafunwa.
Hivyo basi toleo lijalo litaanzia herufi P na litabeba moja ya jina la pipi, peremende, kitafunwa au hata kinywaji. Leo kupitia mtandao wako wa teknokona tutajaribu kuangalia majina nane ambayo mojawapo laweza kuwa ndilo litakalo tumiwa katika toleo la Android P.
Pop-Tarts
Waweza kudhani kwamba jina hili haliwezi kuwa kwa sababu ni jina linalomikiwa lakini kumbuka Android ina majina ya namna hiyo katika matoleo yake mawili ya KitKat na Oreo. Hata hili laweza kuwa Android Pop Tarts.
Pavlova
Ni jina linalofanana na mchezaji maarufu wa muziki aina ya Prima Ballerina wa Russia aliyekuwa akiitwa Anna Pavlova. Pavlova ni jina la kitafunwa kitamu kama keki chenye mchanganyiko wa matunda, mayai sukari na unga wa ngano.
Peppermint
Wengi watakuwa wamejua ni aina ya mmea fulani hivi. Lakini hapa tunazungumzia aina ya pipi inaypondwa kutafunwa mara baada ya chakula cha jioni.
PEZ
Kila mtu anapenda PEZ, ni pipi zenye umbo la matofali kutoka Austria ambazo huliwa kwa kumung’unywa au kutafunwa na wengi wakati wa kuangalia Movie. Ni tamu na zina rangi tofauti tofauti, na mara moja unapoanza kuzila, huwezi kuziacha. Kwa nini Android P isihusisishwe na PEZ?
Popsicle
Kwa kwetu Tanzania ni sawa na kuifanansha na Rambaramba. Ni aina ya malai (Ice cream) ambazo hupendwa sana na watoto. Hii itakuwa na mfanano sana na Android Lollipop
Pancake
Ni aina ya mkate keki ambao hutengenezwa kwa umbo jembamba na duara likiwa na mchanganyiko wa mayai maziwa siagi mafuta na unga wa ngano. Jaribu kusema Android Pancake. Je inasaundi vizuri?
Piña colada
Ni kinywaji kitamu cha mchanganyiko wa tui la nazi, nanasi pamoja na barafu. Pia jina la kinywaji hiki laweza kuwa Android P.
Peda
WAtu wengi hususani wa kutoka India wangependa Google itumie jina lenye asili ya huko. Kuna kitafunwa kitamu kinachofahamika kama Peda cha asili ya India ambacho huchanganywa viungo vya asili, sukari nk.
Google wanaweza kufikiria jina hili kwa kuwa India ni soko la pili kwa ukubwa dunia la simu. Wakati wa Android N liliwahi kupendekezwa jina la kitafunwa la Nankhatai chenye asili ya India lakini jina lilopitishwa likawa Nougat.
Pandoro
Ni aina ya mkate ambao asili yake ni huko Verona, Italia. Ni mkate unaoelezwa umeanza kuliwa tangu karne ya 18. Ni mtamu wenye kutengenezwa mfano wa umbo la nyota na huliwa sana wakati wa Krismasi.
Je Android wanaweza kutumiajina lake. Tusubiri tuone.
Majina mengine ambayo yana nafasi ni Punch, Pineapple, Poached Pears, Pandoro, Praline, Popover, Pastry, Pumpkin Pie, Pecan Pie, Peanut Butter Cookie, Peanut Brittle, Parfait na Panna Cotta