Kuna habari zimeenea ya kwamba tutegemee uwezo wa kuonesha kutufurahishwa na jambo ambalo mtu ameandika au picha aliyoweka kwenye mtandao maarufu wa Facebook kupitia ujio wa kisehemu cha ‘Dislike’ pembeni ya kile cha ‘Like’.
Ni kweli watumiaji mbalimbali wamekuwa wakiomba kampuni ya Facebook kuleta kitufe (button) hicho lakini wiki hii mwanzilishi wa mtandao huo Bwana Mark Zuckerberg amesema hakitakuja kamwe!
Bwana Mark alisema hivyo Ijumaa iliyopita pale alipokuwa katika mkutano huru na waandishi wa habari na wadau mbalimbali, mmoja wa washiriki aliuliza kuhusu ujio wa kitufe hicho. “Tunalifikiria jambo hili”, kisha haraka sana akajisahihisha kwa kusema ya kwamba mtandao huo unatafuta njia mbalimbali za kusaidia watumiaji wake kuzielezea hisia zao lakini si kwa kutumia mfumo wa kitufe cha dole chini (dislike).
Alidai ya kwamba watu kuhukumu ya kwamba alichoweka mtu ya kwamba ni kizuri au kibaya si jambo zuri kwenye jamii yake, hakuna umuhimu wa kuhukumu au kuelezea vitu kwa namna hii bali ni muhimu kutafuta njia zingine nzuri zaidi. Alikubali ya kwamba inabidi waboreshe kwani kuna wakati inakuwa shida mtu kupenda -(Like) kitu alichoandika mwingine kama vile kunusurika kifo, au yupo kwenye wakati mgumu n.k kwani inakuwa inachanganya maana kama mtu atabofya kitufe cha ‘Like’.
Kiuhalisia kwa mtazamo wetu Facebook hawawezi kuja na kitufe hicho kwani kitawatia hofu watumiaji wake pale watakapotaka kuandika au kuweka picha kwenye mtandao huo. Kwani tukubaliane tuu, roho itakuhuma sana kuona umeandika jambo au kuweka picha na watu kukupa kutufe cha kutokupenda ulichoweka. Mwisho wa siku watu wataacha kuandika na hichi si kitu mtandao wa Facebook unaitaji, unataka watu waandike watu wazungumze……
No Comment! Be the first one.