Takribani siku tatu zimepita tangu ndege ya Malaysia Airlines MH17 ikiwa na abiria 297 ikitokea Amsterdam kuelekea Kular Lumapr iangushwe. Ndege hiyo iliripotiwa kuruka kilomita 10 juu ya ardi karibu na kijiji cha Grabovo.
Japo haijulikani ni nani aliyeiangusha ndege hiyo lakini tayari imebainika kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kutoka hewani na gobole. Mpaka sasa, waasi wa nchi Ukraine na Urusi wanashukiwa kushiriki katika ajali hiyo. Hii ni mara ya pili kwa shirika la ndege la Malaysia Airlines kupata majanga, baada ya ndege yake ya MH370 kupotea mwanzoni mwa mwaka huu.
Wataalamu wa mambo ya kijeshi wa nchi za ulaya na marekani wamebaini kuwa inawezekana gobole liitwalo ‘Buk missile’ inayomilikiwa na pande zote zinazoshukiwa kuhusika na shambulizi hilo, lilitumika kutungua ndege hiyo kutoka angani. Gobole hilo limetengenezwa na teknolojia ya Urusi kuanzia miaka ya 1970 na lina uwezo wa kutumwa kutoka ardhini na kuangusha chombo chochote katika urefu wa masafa ya kati angani.
Je, wewe unafikiriaje kuhusu janga hili na matumizi ya teknolojia katika mazingira haya? Umesikia nini zaidi?
No Comment! Be the first one.