Amit Fulay aliyekuwa mkuu katika kampuni ya Google kwenye uzalishaji wa Programu za Allo na Duo ameondoka na kujiunga rasmi na Facebook.
Taarifa ya kuondoka Google na kujiunga Facebook, Amit Fulay aliitoa mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumanne wiki hii.
Amit ni miongoni mwa watu muhimu waliohusika katika kujenga programu ya Hangout, Allo na Duo. Programu zote hizo ni mawasiliano ya watu kwa njia ya ujumbe wa maneno, sauti pamoja na picha za video.
Amit Fulay: Kigogo kutoka Gooogle aliyejiunga na Facebook.
Bw. Amit fulay amedumu katika Google (kampuni) kwa miaka 7 na miezi 5 akiwa sehemu ya watu muhimu waliotoa mchango mkubwa ndani ya kampuni hiyo (Google).
Google hawajazungumza chochote kuhusiana na kuondoka kwa Bw. Amit Fulay na hakuna sababu iliyowekwa wazi ya kuondoka kwake.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.