Katika maeneo ya vijijini, kupata huduma nzuri za elimu ni ngumu. Kwa kutambua hilo, kampuni ya uingereza inayoitwa Aleutia wamebuni darasa linaloweza kuhamishwa na linalotumia umeme-jua. Darasa hilo linaloitwa, “The Solar Classroom in a Box” litaweza kuendesha kompyuta za kusomea zilizoungwa na mtandao wa intaneti bila kutegemea umeme wa gridi ya taifa. Darasa hilo litaweza kutumika na wanafunzi 40 kwa wakati mmoja.

Madarasa haya ya umeme-jua yanayotegemewa kupelekwa katika kila County ya Kenya kuanzia mwaka huu, yanaweza kupanguliwa na kuhifadhiwa nyuma ya gari la ‘pick-up.’ Kwa mujibu wa tovuti ya kampuni ya Aleutia, madarasa hayo yanaweza kusimamishwa na kufanya kazi ndani ya siku moja – bila ya kuhitaji vifaa vikubwa. Lakini darasa litahitaji siku nyingine ya ziada kuhakikisha umeme unafanya kazi, kitu ambacho ni cha kustaajabisha. Kila darasa linakuja na kompyuta 11 zilizotengenezwa kufanya kazi katika mazingira magumu ya joto na vumbi la Afrika. Pia kila darasa lina ‘server’, ‘projekta’ na mtandao wa 3G na satelaiti, vyote vikiendeshwa na umeme-jua unaodakwa kwenye paa la darasa. Darasa hili pia litaweza kuchaji vitu vingine kama simu za mkononi, vitu ambavyo Mike Rosenberg, mwanzilishi wa kampuni ya Aleutia anategemea vinaweza vikaunganishwa kwenye mfumo wa madarasa wanayotengenezwa hapo baadae.
Aleutia ni kampuni inayojikita kwenye kutengeneza kompyuta na teknolojia ya kuboresha afya kwa jamii zinazoendela. Walitengaza hivi karibuni kuhusu suala hili la kupeleka madarasa ya ‘Classroom in a Box’ kwa kaunti 47 za Kenya ili kufikia watoto 20,000. Kwa Aleutia, hii ni nchi ya nane kwa Afrika kampuni hiyo imeweza kuweka teknolojia yao ya ‘Classroom-in-a-box’ . Kwa Kenya, huu mpango wa Aleutia ni mkubwa wa aina yake sasa.
Nchi nyingine Afrika zilizopata kuona mipango kama hii ya elimu kwa kutumia madarasa yanayohamishika ni Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Uganda na Malawi. Tazama video ya mpango huu kwenye nchi ya jirani, Uganda.

Vyanzo: GizMag, The Independent UK
No Comment! Be the first one.