Kwenye ulimwengu wa sasa teknolojia ya kuchaji haraka imeshika kasi kwea makampuni mbalimbali kutoa simu janja ambazo zina uwezo wa kuhimili kujaza umeme kwenye betri ndani ya muda mfupi.
Mimi ni mmoja wa wafuasi wanaopenda sana kifaa cha kidijiti kitumie muda mfupi kuchaji na katika hilo basi pale ambapo mtu ataniomba ushauri kuhusu simu gani anunue rununu ya kisasa ambayo inatunza chaji kwa sana lakini pia haichukui muda mrefu kujaa umeme.
Katika siku za usoni tutarajia ujo wa kimememeshi cha nguvu ya 100W ambacho kitatoka pamoja na simu janja HOnor 50, Honor 50 Pro na Honor 50 Pro+. Kwa mujibu wa dondoo za hapa na pale toleo la Honor 50 na 50 Pro zinaelezwa kuwa uwezo wake wa kuchaji kwa teknolojia ya haraka unaishia 66W.
Kimemeshi cha 100W kitaendana na simu gani?
Kati ya simu janja kutoka familia ya Honor zinazotarajiwa kutoka siku za usoni ni Honor 50 Pro+ ndio inatazamiwa kuwa itakuja na chaji ya uwezo wa 100W. Halikadhalika, simu hii inaelezwa kuwa imewekwa kipuri mama Snapdragon 888.
Kwa upande wa Honor 50 na 50 Pro kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali simu hizi zote kupewa nguvu ya ufanisi na Snapdragon 778G ambayo imetumika kwenye rununu nyingi tuu.
Haya sasa teknolojia ndio hiyo inazidi kupaa jiulize simu janja ninayotumia ina teknolojia ya kuchaji haraka? Ina nguvu kiasi gani upade wa kuingiza umeme kwenye betri?
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.