Tangia Samsung watoe simu janja za kujikunja na kulishangaza soko moja kwa moja makampuni mengine mengi nayo yaliingia katika soko hilo.
Makampuni Kama Motorola, Oppo hata Google waliona nao wasibaki nyuma waingie katika soko hili kwa miguu miwili kabisa katikakufuata nyendo za Samsung.
Licha ya makampuni yanayofanya hivi kuwa mengi sana katika soko lakini bado mpaka sasa kampuni ya Samsung ndio inaongoza kufanya vizuri katika soko.
Ni wazi kwamba ni kampuni kubwa sana la kiteknolojia na limekua likiuzia vipuri mbalimbali kwa makampuni menzake ya teknolojia hata kwa wapinzani wake wakubwa, Apple.
Mpaka sasa bado kampuni ya Apple bado haijaingiza katika soko kifaa chochote ambacho kina kioo cha kujikunja kama washindani wao Samsung.
Kwa fununu ambazo zipo kwa sasa ni kwamba kampuni ya Apple iko katika mchakato wa kuja na kifaa chenye kioo cha kujikunja.
Sasa basi kwa haraka haraka ni kwamba kioo hichi kitapatikana moja kwa moja kutoka katika kampuni ya Samsung na LG ambao wanasifika sana kwa kutengeneza na kuuza vioo vya aina hii.
Fununu ni kwamba Samsung na LG wanawaandalia Apple kioo cha inchi 20 mpaka 25 ambacho kitakua mahususi kwa ajili ya kifaa cha aina hiyo.
Kumbuka hata kwa sasa Samsung ndio msambazaji mkubwa wa vioo vya OLED kwa Apple, kwa hiyo hili litawezekana kiurahisi tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kifaa cha kwanza cha Apple cha kujikunja kitakua ni nini?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.