Kufahamu kama una viambukizi vya HIV au kisonono ndani ya dakika 15 tuu!!!! Kifaa hichi kidogo kitaitaji kuunganishwa na simu yako janja kupitia sehemu unayotumia kwa ajili ya waya za spika (earphone).
Teknolojia inazidi kukua na kukua kwako kunasaidia kupunguza ukubwa wa vifaa, na pia bei ya vifaa vinavyofanya kazi hiyo. Si unakumbuka simu zilivyokuwaga kubwa na za bei ghari? Sasa pia kifaa kinachoweza kukupa majibu ya kama una HIV au kisonono kimetengenezwa na kama kikiingia sokoni kitaweza kuuzwa kwa tabribani Tsh 60,000/= (dola 34 za Marekani).
Je wamewezaje kutengeneza kifaa kwa bei rahisi hivi?
Kitu kikubwa zaidi ni kwamba kuna teknolojia nyingi sana kwenye simu yako janja, na kupitia simu hili wameweza kutoa vitu vyote ambayo si vya lazima kuwekwa kwenye kifaa hicho cha kupimia ambavyo vipo tayari kwenye simu janja. Wametengeneza kifaa ambacho kitafanya vipimo vya mwanzo zaidi ila kwa mambo mengine makubwa zaidi yatafanyika kupitia simu yako janja kwenye App yao maalumu.
Kinafanyaje kazi?
Kuna sehemu ya wewe kuweka damu yako kidogo, kisha kuingiza kwenye kimashine hicho. Yote hii ikiwa kifaa hicho umekiunganisha na simu janja ya iPhone au Android yenye app yao maalumu. Baada ya dakika 15 utapata majibu.
Kifaa hicho ambacho kishafanyiwa majaribio nchini Rwanda kinasemekana kina ubora mzuri tuu kama vifaa vingine vikubwa na ghari vinavyotumika sasa. Kwa sasa Tiffany Guo na Tassaneewan waliokuja na teknolojia hiyo wanatazamia teknolojia yao ikubaliwe na shirika la Afya duniani (WHO), teknolojia hii ikipitishwa na WHO basi itaweza kutengenezwa kwa wingi na kuingia sokoni.
Kwa kifupi tutegemee ata mtu mmoja mmoja kuweza kununua na kukaa chumbani na kujipima.
No Comment! Be the first one.