Sasa watumiaji wa Facebook hawatalazimika kuchagua LIKE katika posti za marafiki zao Facebook, na badala yake wataweza kuchagua Kupenda, Kuchukia, Kucheka, Kushangaa au kuhuzunika kwa kutumia Emoji mpya za hisia zitakazoambatanishwa katika marekebisho makubwa ya kitufe cha Like yanakayofanywa na Facebook.
Hayo yalitambulishwa jana na mwanzilishi wa mtandao huo, Mark Zuckeberg kupitia ukurasa wake wa Facebook, akiweka video iliyotambulishaujio wa vitufe hivyo vipya vinavyotazamiwa kuwa na nguvu kubwa kwa watumiaji wa mtandao huo.

“Tumechunguza aina ya comments na hisia zinazoonyeshwa kwenye posti mbalimbali na kugundua kuwa zainafanana ulimwenguni kote. Watu wote wanacheka, kuchukia, kushangaa n.k. Sasa tutawawezesha waweze kuonyesha hisia zako kwenye kurasa zao za Facebook.” Anaelezea Chriss Cox, mkuu wa bidhaa za Facebook.
Vitufe hivi vitakuwa vinatambulika katika tamaduni zote Ulimwenguni kwa sawa, ili kuwezesha wote kuwa na hisia za aina moja wakati wa kuchangia katika posti za marafiki wote duniani.

Watu wengi wamekuwa wakisubiri Facebook walete vitufe vitakavyoweza kuonyesha hisia tofauti za zile za kitufe cha LIKE pekee, ili kuonyesha hisia hasi kama kuchukia, kuhuzunika au kucheka.
Kwa wakati huu, vitufe hivi vya hisia vitapatikana kwa majaribio kwanza katika nchi za Spain na Ireland, kama kukiwa na mafanikio zitaachiliwa kwa Ulimwengu mzima.
Baada ya saa 11 ya kuchapisha video hiyo kutambulisha vitufe vya hisia mtandaoni, zaidi wa watu Laki Tisa walipenda posti hiyo ya Zuckerberg, ishara tosha kuwa unasubiriwa kwa hamu na kukubalika kwa jamii.
Watumiaji wa Facebook sasa wateweza kuchagua labda Kupenda, Kushangaa, Kuhuzunika au Kuchukia katika posti za rafiki zao. Haya ni zaidi ya walichopendekeza, kwani mwanzo walipendekeza kitufe cha Dislike kiongezwe kama tulivyochapisha siku za nyuma katika mtandao huu.
Huu ni mfululizo wa maboresho makubwa yanaoendelea kufanywa na Facebook baada ya kutambulishwa kwa mifumo mingi mipya ya mtandao wa Facebook, ili kuendelea kuongeza idadi ya watumiaji duniani.
2 Comments