Ni wazi kwamba mpaka sasa kuna vivinjari vingi sana na makampuni mengi ya teknolojia yanamiliki vivinjari hata wao Samsung hivyo hivyo.
Ukichana na kivinjari cha Samsung, kampuni ambayo inaongoza kwa kivinjari chenye watumiaji wengi ni Google ambacho kivinjari chake ni chrome.
‘Samsung Internet’ ni kivinjari ambacho kilikua kinapatika bila ya kushusha katika vifaa vya Samsung sana sana katika simu janja na tabiti.
Kivinjari hiko kwa sasa kimeanza kupatika katika soko la App la Microsoft (Microsoft store) kinapatikana kwa Windows 10 hata Windows 11.
Kingine ni kwamba kampuni imefanya hivyo kimya kimya bila ya kupiga kelele nyingi na pia kivinjari hiki hakina tofauti kubwa ya kimuonekano na Google Chrome pia.
Ni wazi kwamba kuna vivinjari vingi sana na kuna vinavyopendwa kuliko vingine kama Samsung nae kaamua kuweka chake katika masoko mengine inamaana anaingia katika ushindani.
Hongera kwa kampuni, japo wao kwa wao hawajatoa tamko lolote kuhusiana na jambo hili lakini inaonekana lina maana kubwa na mara nyingi makampuni makubwa hayafanyagi vitu bila sababu hata kama sababu haijawekwa wazi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kivinjari hiki kilitaleta ushindani mkubwa kwa vingine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.