Toleo lijalo la moja ya programu maarufu zaidi ya uendeshaji (Operating System – OS) linalotengenezwa na Microsoft – Windows 10 linazidi kunukia.
Ila kutokana na ukweli ya kwamba mambo mengi zaidi yamezidi kufanyika katika utengenezaji wa OS hii kiteknolojia na kama ilivyokawaida katika ulimwengu wa teknolojia za programu uendeshaji si vifaa vyote vilivyokuwa vinatumia toleo lililopita la OS vitaweza kutumia Windows 10 ufanisi mzuri wa bila matatizo.
Yaani ili kompyuta au tableti iweze kutumia toleo hili jipya la Windows basi lazima iwe inasifa flani flani na Microsoft wamezitaja.
Kumbuka hiki ni kiwango cha chini kabisa lakini unashauriwa uwe na kiompyuta yenye uwezo mkubwa zaidi ya huu kulingana na bajeti yako.
Sifa hizo ni si chini ya;
RAM – ‘Memori’, GB 2 kama utaweka tolea la Windows 10 64 bit na GB 1 au kama utataka kuweka toleo la Windows 10 32 bit.
Diski Uhifadhi (Hard Disk)
– GB 16 au zaidi kwa toleo la 32 bit
– GB 20 au zaidi kwa toleo la 64 bit
Kwa watumiaji wa tableti zinazotumia Windows kama vile Surface na nyinginezo basi tableti inatakiwa iwe na kibonyezo (button) vya Kuzima na Kuwasha (Power button) na kibonyezo cha kuongeza na kupunguza sauti. Ila pia uwezo wake kwenye RAM na diski uhifadhi inatakiwa iwe na sifa kama tulizozitaja hapo juu.
Zaidi ya hapo pia lazima kompyuta/tableti yako iwe na sifa nzuri ya kadi ya kimuonekano (Graphics) inayokubali programu ya DirectX 9 kutoka Microsoft. Laptop na tableti nyingi za kisasa zinazotumia Windows zinasifa hii.
Je vipi kuhusu simu zinazotumia matoleo ya Windows 8.*?
Vibonyezo vya kuwasha na kuzima, na vya sauti ndiyo vinaitajika. Pamoja na sifa hii pia lazima simu iwe na RAM si chini ya GB 4, kwa ufupi sana inasemekana kama simu yako inatumia tolea la Windows 8.1 basi ndiyo kabisa usiwe na wasiwasi kwani utaweza kusasisha (update) kwenda tolea la Windows 10 bila shida yeyote.
Ila pia baadhi ya simu zenye RAM kiwango cha chini ya GB 4 wataweza pata toleo ili ila hii ikiwa tuu vioo vyake vikiwa ni vidogo zaidi.
Tuitegemee lini?
Vyanzo vinasema tuitegemee kuzinduliwa na kuanza kupatikana rasmi kuanzia mwishoni wa mwezi wa 6.
Itakuwa BUREEEEE!
Ndiyo ila tuu kama tayari unatumia matoleo ya Windows 7 na Windows 8. Utaweza kusasisha kwenda toleo jipya bure kwa muda wa mwaka mmoja kupitia intaneti. Baada ya hapo itakubidi kuilipia kama utaitaka.
Itakuwaje kama unatumia tolea la wizi la Windows 7 au 8?
Microsoft wamesema watawapa nafasi ya kusasisha (upgrade) kwenda Windows 10 ata wale wanaotumia programu hiyo kiwizi. Wanategemea baada ya muda watu kama hawa itakuwa rahisi wao kulipia baada ya kuona faida ya kutumia programu isiyo ya wizi. Inasemekana katika watumiaji 10 wa toleo la Windows nchini China ni 1 tuu ndiye ameipata kwa kununua.
Kuifahamu Windows 10 Zaidi Bofya hapa -> Windows 10
Endelea kutembelea TeknoKona na usisahau kusambaza makala hii kwa ndugu na marafiki!! Ungana nasi kwenye mitandao mingine ya kijamii kwa kubofya hapa chini
No Comment! Be the first one.