Kuacha kazi….Siku ngumu, mbaya au hata ile inayokuacha na mawazo mengi katika kipindi cha kazi inakufanya utamani hata kupigwa ngumi ya uso kuliko mateso unayoyapata moyoni. Mara nyingi siku hiyo itakuacha ukijiuliza maswali mengi, na ni vizuri kujiuliza maswali mengi kama maswali hayo yanahusisha kulipwa kwako (ahah!).
Kabla hujahamaki na kumfuata bosi wako na kumuambia ‘Kazi yako Nakuachia nkah!’ kuna vitu inabidi ujiulize kwanza ili kupata uhakika kwamba uache kazi hiyo au la. Moja kati maswali ya muhimu ya kujiuliza ni kwamba Je, una pesa ya kutosha kujikimua angalau mpaka utakapo pata kazi nyingine au hata ambayo inaweza ikakufikisha miezi sita bila kulipwa?
Maswali mengine yanweza yakawa yale ya ndani kwa ndani kwa mfano Je, ujuzi wako unahitajika sana katika soko la ajira? Maswali yako mengi sana na kabla hayajakuchanganya hivi unaweza ukawa hujui cha kufanya kabisa.
Hapa sasa ndipo mtandao huu unapokuja kufanya kazi,unaitwa ‘Should I Quit My Job?’ (Tafsiri: Je, Niache Kazi?) na kazi yake kubwa ni kukupa akili ya ziada juu ya swali hilo.

Ndani ya mtandao kuna maswali 25 ambayo ni tofauti ambayo itakubidi uyajaze. Kulingana na wewe na kazi yako mlivyo kuna maswali ya kukubaliana nayo na kuna mengine ya kupingana nayo. Ukishamaliza kuyajibu yote mtandao utakupa majibu yako
Majibu hayo yatakuwa katika ushauri wa aina tatu ambayo ni ; stay, go, look for another job before quitting (Tafsiri: Bakia, Ondoka , Tafuta kazi nyingine kwanza kabla ya kuacha kazi).
Utapata jibu moja kati ya hayo, ukishalipata ndipo hapo utaanza kulifanyia kazi. Watu wengi wanapatwa na changamoto za kufanya kazi ambazo hawazipendi. Mbaya zaidi wanashindwa hata kuondoka katika kazi hizo juu ya sababu mbalimbali za kimaisha. Lakini huwezi jua kama utatumia mtandao huu unaweza ukawa ndio mkombozi wako
Ingia Katika Mtandao Wa https://www.sokanu.com/should-i-quit-my-job Na Uanze Kujibu Maswali au kwa haraka bofya hapa…