Chonde chonde, kuweni makini mkiwa mnachaji simu. Wakati siku chache zilizopita familia moja China ililalamika kuwa binti yao alifariki kutokana na kupigwa shoti wakati anatumia simu ya iPhone ikiwa kwenye umeme, habari zingine zimetokeza kuhusu mwanaume ambaye yupo hospitali tokea tarehe 7 mwezi huu kwa ajili ya aina hiyo hiyo. ya ajali.
Binti wa miaka 23, Ma Ailun alikuwa ni bibi harusi mtarajiwa wa kuolewa tarehe 8 mwezi ujao alikufa pale alipopigwa shoti ya pale alipopokea simu yake ilipoita bila kuitoa kwenye chaja yake. Na sasa habari imejitokeza kuwa kuna mkaka ambaye amelazwa hospitali huko huko nchini Uchina tokea tarehe 7 mwezi huu baada ya kupigwa shoti pale alipopokea simu yake ya iPhone ikiwa bado kwenye chaji.
Je Ufanyaje?
Cha kwanza inasemakana wote hawa walikuwa wanatumia chaja ambazo hazitambuliki ki-kiwango, kama mnavyojua tena bidhaa za Uchina. Hivyo ushauri kutoka Teknokona ni kwamba kama unatumia simu za iPhone au zingine zozote hakikisha unanunua chaja zenye viwango na epuka kitu kisa bei rahisi sana mfano seti nzima ya chaja halisi za iPhones kutoka Apple zinaweza patikana kwa zaidi ya Tsh 40,000/= lakini zile zisizo rasmi utazipata kwa chini zaidi. Lakini ujiulize usalama je?
No Comment! Be the first one.