YouTube inatarajia kuondoa uwezo wa kuchati kwenye app yao. Uwezo huo wa kutumiana ujumbe binafsi (kuchati) ulianza rasmi miaka ya 2017 na unaondolewa sio kwa sababu za kutotumika bali kwa sababu za kiusalama zaidi.
Uwezo wa kuchati uliletwa kwenye YouTube ili kuongeza uwezo wa watu kutumiana video za kwenye mtandao huo (links) na kufanya mazungumzo binafsi kuhusu kile wanachotazama n.k. Uondoaji huu unaonekana ni kwa sababu za kiusalama zaidi na kwa lengo la YouTube kuendelea kufanya huduma yao kuwa ya watu wote bila kujali umri.
Kwani kwa kutofanya hivyo kumekuwa na malalamiko utumiaji YouTube kwa watoto umekuwa ukipanda na hivyo wazazi wanakuwa na wasiwasi kuhusu watu wanaoweza kuchati na watoto wao kupitia eneo la kuchati.
Taarifa hii imetolewa na YouTube kwenye ukurasa wao – youtube
Hatua hii imewafanya watumiaji wengi asa vijana kulalamika kuwa sasa hawatoweza kuwasiliana na rafiki zao kwa kuwa wengi wamekatazwa kutumia mitandao mengine kutokana na umri wao asa nchi za Marekani na Uingereza.