Mara nyingi tunapoangalia filamu katika lugha ambayo hatuwezi kuiongea kiufasaha, kwa kawaida huwa tunakabiliwa na matatizo ya uelewa ni nini huwa kinasemwa katika filamu husika. Hapo ndipo pale subtitles huwa mkombozi wetu katika kuelewa kile waigizaji wanaongelea bila kujali lafudhi yao.
Kama wengi tulivyo na ufahamu kuwa kuna tovuti nyingi kwenye intaneti ambazo unaweza kupakua subtitles bure. Mara baada ya kupakua nakala ya subtitle unaweza kuihamishia kwenye folder la filamu husika na programu nyingi zinazotumika kucheza video zinaweza kupakia nakala hiyo moja moja kwenye filamu husika. Lakini unaonaje kama VLC ikapakua nyakala za subtitles moja kwa moja kwa ajili yako?
Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza pakua na sakinisha(install) toleo jipya la programu ya VLC Media Player kwenye tovuti tovuti yao rasmi.
Hatua ya pili
- Baada ya kusanikisha toleo jipya la VLC Media Player fungua filamu unayotaka kuitazama kisha nenda kwenye kichupo(tab) cha ‘View‘
- na Bonyeza kitufe cha ‘Download Subtitles‘
Hatua ya tatu
- Katika dirisha la VLsub lililofunguka andika jina la filamu na bonyeza ‘Search by name‘ na orodha ya nakala za subtitles zilizopo itatokea.
- Chagua nakala ya subtitle uitakayo katika orodha kisha bonyeza kitufe cha ‘Download Selection‘ baada ya sekunde kadhaa nakala ya subtitle itapakuliwa na kupakiwa ndani ya filamu
Hii ni moja ya njia nyepesi na rahisi ya kupakua subtitles kutoka kwenye intaneti kwa haraka zaidi.
Tuambie maoni yako kupitia eneo la comments, na kama kuna maujanja yoyote ungependa tukuambie siku za mbeleni katika mtandao wako wa TeknoKona.