USB Ports za kwenye kompyuta zetu zinaweza kuwa chanzo cha kompyuta zetu kushambuliwa na virusi kutokana na kuruhusu ata vifaa vya USB flash tusivyovifahamu kutumika saa nyingine bila idhini yetu.

Je, ufanye nini kuzuia mtu mwingine yeyote kutumia USB Flash kwenye kompyuta yako na hii ikiwa mara nyingi bila ya kuwa na ata uhakika wa kwamba flash hiyo haina virusi? Leo jifunze namna ya kufunga/kufunga USB ports za kwenye kompyuta.
Zipo njia mbalimbali zitakazokuwezeshesha kufunga au kufungua ports za kwenye kompyuta lakini kwenye makala hii nitakuelekeza hatua kwa hatua njia rahisi ya kuzifanya ports zako kutokuwa chanzo cha virusi kwenye kompyuta yako.
>Bofya “Window Key+R”.
Window Key+R ni njia fupi na ya mwanzo kabisa kuweza kufunga/kufungua ports za kwenye kompyuta ila unaweza ukabonyeza kitufe cha “Start” na kisha ukaandeka neno Run>>OK.

>Tafuta neno “HKEY_LOCAL_MACHINE\SYSTEM\CurrentControlSet\Services\UsbStor”.
Hapa ndipo umakini wa hali ya juu unahitajika kwani ndio kiini cha zoezi zima la kuweza kufunga/kufungua ports za kwenye kompyuta. Ukishindwa kufika kwenye hatua hii basi utakuwa umeshindwa kutimiza adhma ya kuweza kuzilinda ports za kwenye kompyuta yako.

>Weka namba 0 au 4 kwenye kiboksi.
Ndio, sasa hapo utakuwa umekaribia kukamilisha zoezi zima. Ukiwa umebonyeza mara mbili (double click) kwenye neno “Start/Capabilities” (kwenye hatua iliyopita) kuna kiboksi kinatokea hapo utaona inasomeka namba 4 (ikimaanisha ports zako zinafanya kazi).

Njia mbadala ya kufunga/kufungua ports za kwenye kompyuta.
Ukishabofya Window Key+R kuna kiboksi kitatokea na hapo utaandika “devmgmt.msc”. Orodha ndefu itatokea, tafuta neno Universal Serial Bus controller. Kisha ukitaka kuzima baadhi ya ports ni muhimu basi unaweza ukachomeka na kuchomoa kitu kwenye port ili kuona mabadiliko ya port husika kutokea kwenye skrini ya kompyuta.

Ni mhimu sana kuacha wazi zile ports ambazo unazitumia mara kwa mara ili kuepusha komoyuta yako kushambuliwa na virusi vilivyotokana na kuchomeka USB flash mbalimbali. Washirikishe na wengine wapate kuelimika kama wewe.
Vyanzo: The Windows Club, ccm.net