Tangu kuwepo na mkazo kutoka mamlaka husika, watu wanaotumia king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice Tanzania wateja wake hawaoni tena chaneli za ndani kwenye DSTV mpaka hivi leo.
Nikiwa kama mkereketwa wa suala zima la kukosekana kwa matangazo ya chaneli za ndani kwenye DSTV ilinibidi nifanye kila jitihada kuweza kupata ukweli na muhstakabali kutoka mahali sahihi na kwa kweli nikapata kuelezwa ambacho kipo na ilivyotakiwa kuwa tangu huko nyuma.
King’amuzi cha DSTV kinapata matangazo ya chaneli zake kutoka kwenye satelaiti na iwapo zile chaneli zitajumuishwa upande huo itabidi makampumi yanayomiliki chaneli hizo waachane na mfumo wa kurusha matangazo bure; hii ikimaanisha itamaanisha:-
- itabidi wakate leseni mpya ambayo ni ghali kulinganisha na ya sasa lakini kubwa zaidi waache mitambo ambayo inawezesha matangazo hayo kupatikana,
- zikihamia (chaneli za ndani) kwenye DSTV hawatakuwa na haki ya kurusha matangazo ya makampuni mbalimbali kwa sababu DSTV inaweza kuonekana nje ya Tanzania na tangazo hilo likionekana nchi za serikali ya Tanzania itaingia gharama ya kulipia tangazo husika kutokana na kwamba limeonekana kwenye nchi hiyo bila kulipiwa,
- hata idadi ya wafanyakazi kwenye kampuni husika itapungua kwa sababu mambo mengi yatakuwa yakitokea kwenye satelatiti hivyo hakutakuwa na haja ya kuwepo kwa baadhi ya waajiriwa.