Simu zetu zinatusaidia kwa mengi tu na zimetokea kuwa msaada kweli kweli katika mambo mbalimbali hasa katika dunia ya kileo. Sasa jambo la kukosea namba linaweza kuwa la kufedhesha lakini pia linaweza kugeuka na kuwa neema.
Hebu fikiria ni mara ngapi umekosea namba ya simu halafu akapokea mtu ambaye sio yule uliyetegemea? Binafsi nimeshakosea mara nyingi tu 😀 😀 😀 . Binti mmoja alikosea namba lakini sasa ndio amekuwa mumewe 😯 😯 😯 .
Bi. Lalita Ben Bansi, 26 ambaye pia ni muathiriwa wa shambulio la tindikali na kufanyiwa upasuaji mara 17 nani alifikiri kuwa angeweza kupata mpenzi? Lakini hilo ni historia sasa kwani ameweza kupata mume.
Wawili hao walikutanaje?
“Bi Bansi alipiga simu yangu kwa bahati mbaya miezi mitatu iliyopita. Alimpigia tena baada ya siku 15. Walizungumza na akatokea kuipenda sauti ya Bw. Singh, mwenye umri wa miaka 27, anayefanya kazi na kampuni ya CCTV. Waliendelea kuzungumza kila siku na ni hapo ndipo akamuomba kumuoa; nchini India wanawake ndio wanaoa na si mwanaume kama huku kwetu Afrika!
Wakati wa mazungumzo yao, Bi Bansi alimueleza Bwana Singh kwamba yeye ni muathiriwa wa shambulio hilo la tindi kali baada ya kushambuliwa na jamaa yake mwaka 2012.
Hatua ya Bi. Lalita imechukuliwa kama “Hatua ya kishujaa” hasa ukizingatia na makovu aliyonayo kwenye sura yake. Wachumba wengi hupendana kwa sababu ya sura na miwshowe huishia kutalakiana. Lakini kwa Bw. Singh ilikuwa ni tofauti kwani hakuvutiwa na sura, yeye (mkewe) ni mtu mzuri.
Soma pia: Aachwa saa chache baada ya harusi yake kisa kuchati
Harusi yao ilihudhuriwa na nyota wa filamu za Bollywood akiwemo muigizaji Vivek Oberoi, aliyekutana na Bi. Bansi katika hafla iliyoandaliwa kwa waathiriwa mashambulio ya tindikali.
Hakika hakuna kinachoshindikana chini ya Jua, kasoro uliyonayo isikuvunje moyo ukasita kufanya kile unachokiweza. Kuwa mlemavu haimaanishi huwezi kitu. Endelea kutufuatilia kupitia Facebook, Twitter, Instagram.
Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali