Ni wazi kwamba kampuni za magemu zinafanya vizuri sana kwa kipindi hichi na ni wazi kwamba makampuni kama vile Xbox na Nintendo yanaweza nunuana kama yakifikia makubaliano.
Nintendo ni moja kati ya kampuni kubwa sana katika Nyanja nzima ya magemu na kwa taarifa zilizotoka zimeonyesha dhahiri kwamba walikua na mpango wa kulinunua kampuni la Nintendo na Valve.
Kama unakumbuka Microsoft ilitoa dili nono la kuinunua kampuni ya magemu Activision Blizzard ambalo dili hilo mpaka sasa halijakamilika sababu ya kesi iliyopo
Baadhi ya nyaraka ambazo zimetolewa kama sehemu ya ushahidi katika mahakama zimeonyesha kwamba Xbox ambayo inamilikiwa na Microsoft ilikua na mpango wa kununua makampuni hayo mwaka 2020.
Katika moja ya barua pepe kutoka kwa mkuu wa Xbox (bwana Phil Specer) na upande wa Nintendo ambako alikua akiongea na mkuu wa masoko wa kampuni hiyo bwana Takeshi Numoto.
Barua pepe hiyo ilikua na kichwa cha habari kinachosomeka “random thoughts’ ikiwa na maana ya mawazo ya aina mbali mbali kwa haraka haraka.
Dhumuni lake ilikua ni kutaka kuona kama Xbox itaweza kuinunua kampuni hiyo ya Nintendo na kuifanya kuwa chini yake.
Mpaka sasa ni wazi kabisa kwamba kama ingetokea dili hilo lingefanikiwa basi lingekua ni la mapinduzi makubwa katika tasnia nzima ya magemu.
Katika mazungumzo hayo mengi hayajawekwa wazi kuhusiana na Valve lakini liko wazi kwamba na wao walikua wanawindwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako je unadhani kama Nintendo wangefanikiwa kununuliwa na Microsoft leo wangekua wapi? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.