Hivi ni mara ngapi umejaribu au umekuwa ukimuhadisia mtu kuhusu ‘Movie’ Fulani lakini ukawa hukumbuki jina lake? Kwa kutumia mtandao huu hilo halitakuwa ni tatizo tena
Mda mwingine unaweza ukamuhadisia mtu ‘movie’ Fulani uliyoiona lakini ukajishangaa tuu hukumbuki vizuri jina lake na ukajikuta unatoa jina la ‘movie’ nyingine kabisa.
Kwa kutumia mtandao wa whatismymovie.com hilo halitakuwa tatizo kabisa. Mtandao huu utakusaidia kujua jina la ‘Movie’ yako
Jinsi ya kutumia mtandao huu ni rahisi sana kwani itakubidi uandike baadhi ya maneno au uelezee kidogo jinsi movie hiyo ilivyo au nani ameigiza na ameigiza vipi. Maneno haya ni vizuri yakawa katika sentensi moja tuu.
Katika mtandao huo ukiufungua utakuatana na sehemu ya kutafuta (search) amabapo itakubidi kuandika maelezo yako kuhusiana na ‘Movie’ hiyo. Maelezo hayo yanaweza yakawa yanaelezea waigizaji, waandaaji, aina ya ‘Movie’ na kuendelea. Kwa mfano unaweza ukaandika
itakuletea ‘Movie’ ya Keanu Reeves, Knock Knock
Baada ya ku ‘click’ tafuta (search) itatokea list kubwa tuu ikihusisha majibu ambayo yanahusiana na ulichokiandika (kukitafuta). Ukitaka kupata majibu sahihi kabisa mtafutaji anaweza aka’click’ eneo ambalo limeandikwa “Good Match” kama alichokitafuta amekipata au aneweza aka’click’ kwenye “Bad Match” kama alichokitafuta hakijatokea kama alivyokuwa akitarajia
Majibu yako yatahusisha jina la ‘Movie’ hiyo pamoja na mwaka ilipoachiwa, kava lake na maelezo mafupi juu yake.
Matandao wa whatismymovie.com umeanzishwa na kampuni ya Valossa. Pia mtandao huu hauna kazi ya kukuambia jina la ‘movie’ tuu bali pia inaweza ikakuambia ‘movie’ gani ya kuangalia kwa mfano unaweza ukaandika “Find all Avengers Movies” na mtandao utaleta zote za Avengers hii itakusaidia kama kuna zile ulizoziruka katika mtiririko huo kuweza kuzitafuta na kuziangalia.
Hayo ndio maajabu ya Teknoloojia, karibia kila siku kinawezekana siku hizi, bado inazidi kukuwa kwa kasi. Kwa kutumia njia hii unaweza ukapata msaada wa nguvu tuu kuhusiana na ‘Movie’.