Si mara zote unaweza kupata picha nzuri kwa kutumia simu yako, tunafahamu kuna baadhi ya simu zinasifika kwa kupiga picha nzuri na zenye ubora mkubwa. Lakini ni vyema uwe unajua namna ya kuweka mipangilio (settings) vizuri ili upate matokeo mazuri unayoyategemea.
Kumbuka kuna watu wana simu nzuri sana, ila bado picha wanazopata huwa si nzuri – kuna muda kosa si simu bali ni mipangilio ambayo mtumiaji simu ameweka.
1. SAFISHA KAMERA (CAMERA LENS) KWENYE SIMU YAKO.
Simu inatumiwa mara nyingi na unaweza kuishika sehemu ya kamera kila mara utumiapo, simu inaweza kukusanya uchafu kama vumbi au mafuta na kupelekea kutoa picha zenye ukungu/blurred images, kabla hujaanza kupiga picha hakikisha unaisafisha kwa kitambaa kisafi na kikavu.
2. BADILI QUALITY/UBORA WA PICHA KWENYE MPANGILIO (SETTINGS).
Ubora au Quality ya picha iweke kwenye hali ya muonekano angavu wa hali ya juu (High resolution) sio kenye ung’avu wa kati (standard) wala ung’avu wa chini (low) maana unaweza kuhitaji kuichapisha/print kwa matumizi ya baadae na ikiwa na ung’avu wa chini (low resolution) hautaweza kuichapisha (print) ikatoka vizuri.
3. USITUMIE MIPANGILIO YA KAMERA(CAMERA EFFECTS) INAYOWEZA KUHARIBU PICHA.
Usitumie mipangilio ya camera (camera effects) zinazowezakuharibu picha mipangilio hiyo ni kama black-and-white, sepia tones, inverted colours na badala yake tumia original effects tu na ukitaka kuhariri (editing) yafaa zifanyike kwenye app/programu maalumu kama Light room, Adobe photoshop.
4. TUMIA TOCHI YA SIMU (FLASHLIGHT) PANAPOHITAJIKA.
Tumia tochi ya simu/flashlight panapotakiwa na mara nyingi hii hua ni otomatiki (auto), vifaa vya kamera ambavyo huitwa sensor hua zinatambua (detect) kwamba hakuna mwanga wa kutosha basi tochi/flash light ndio hutokea, usilazimishe kuweka tochi/flash kwenye mazingira ambayo sensor haijatambua (detect) uhafifu wa mwanga.
Fahamu kuhusu apps nyingine mbalimbali -> Teknokona/Apps
No Comment! Be the first one.