Kurasa za mitandao za kijamii za mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg zadukuliwa.
Akaunti zake za mtandao wa Twitter, LinkedIn na Pinterest zilidukuliwa na kutekwa kwa muda siku ya Jumapili kabla ya wataalamu wa usalama wa mitandao kumudu kuzidhibiti saa chache baadaye.

Kundi la wadukuzi la “Ourmine” limedai kudukua akaunti za Zuckerberg. Kundi hilo lilijigamba kwenye ujumbe waliochapisha kwenye mtandao wa Twitter kuwa ndio waliodukua kurasa hizo na wakamtaka Zuckerberg awatumie ujumbe wa moja kwa moja iwapo alikuwa anataka umiliki wa akaunti hizo.
“Vipi @finkd tumeingia kwenye akaunti zako za Twitter, Instagram na Pinterest, tuna’test’ kiwango chako cha usalama tuu, tafadhali wasiliana nasi”.

Ujumbe huo hata hivyo umefutwa kwa sasa. Japo anaimiliki ukurasa huo lakini Zuckerberg hajachapisha ujumbe wowote tangu mwaka wa 2012.
Wandani wa maswala ya usalama wa mitandao ya Intaneti wanadai kuwa huenda udukuzi wa mwaka wa 2012 wa ukurasa wake wa LinkedIn ndio uliochangia tukio hilo la jana. Kosa likiwa ni kutobadili password yake kwa muda mrefu sana, na hivyo password yake ya LinkedIn ndiyo iliyotumika kuingilia kwenye akaunti zake za Twitter, Pininterest na LinkedIn.
Ingawa ana akaunti Twitter si mtumiaji sana. Ingawa wadukuzi hao walidai ya kwamba waliingia hadi kwenye akaunti yake ya Instagram wenyewe Instagram wamepinga na inasemekana ni kweli hawakufanikiwa katika hilo.
2 Comments
Comments are closed.