Mfumo wa majaribio ya kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole (Biometric) vya watumiaji umezinduliwa rasmi, tarehe 1 Machi, jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo litahusisha kwa sasa mikoa ya mikoa mitano ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar. Mikoa itakayohusika na mpango huo kwa awamu hii kwa Tanzania Bara ni Iringa, Tanga, Singida, Pwani na Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo katika viwanja vya mnazi Mlimani City, Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema utumiaji wa simu za mkononi umekuwa na udanganyifu katika kutoa taarifa za wanaosajili namba zao huku wengine wakitumia
simu kufanya uhalifu.
Aliongeza Ili kuondokana na changamoto hizo na pamoja na kupata takwimu halisi ya ya watumiaji wa simu za mkononi kwa ajili kuweka mipango ya kuendeleza sekta ya mawasiliano wanalazimika kuanza mfumo huo wa usajili kwa alama za vidole.