WhatsApp sasa imeanza kuruhusu watumiaji wake kutumiana documents, katika toleo lake lililotoka Jumatano asubuhi kumeongezwa uwezo wa kutuma na kupokea mafaili ya PDF.
Wapinzani wakubwa wa mtandao huu kama vile Telegram wamekuwa na huduma hii kwa muda mrefu na pengine hii ni hatua ya makusudi kutoka kwa WhatsApp kupambana na wapinzani.
Mabadiliko haya yanakuja na update iliyotoka mapema Jumatano, kama haujaanza kuona huduma hii mpya basi unatakiwa ku-update app yako. Mabadiliko haya yamekuja kwa pamoja kwa watumiaji wa iOS pamoja na Android (Ha!ha! mambo ya haki sawa), na pamoja na kuongezwa huduma ya kusambaza mafaili pia kuna mabadiliko machache kwenye muonekano wa WhatsApp.
Kupata Mabadiliko haya ni lazima kupakua toleo jipya la WhatsApp ambalo tayari lipo katika soko la app la playstore, ama kama kwa namna moja ama nyingine playstore haikupi toleo jipya zaidi la WhatsApp basi unaweza kupakua toleo la app hii la APK ambalo linapatikana HAPA (Soma kwanza jinsi ya ku install app kwa katika mfumo wa APK ).
Baada ya kuwaumeisha shusha na kuinstall toleo jipya zaidi la WhatsApp yako ukiifungua na kwenda sehemu ya kuambatanisha media (pale ambapo huwa tunaenda kwaajiri ya kuambatanisha picha ama muziki) kisha unatakapofungua utaona kuna vipengele sita (Ndio hata kabla ya update vilikua vipengele sita ila ni kwamba sasa hivi kipengele cha video na photo vimeunganishwa na kutengeneza kipengele kimoja cha camera) ambapo kimoja kimeandikwa documents hiki ndicho hasa ambacho kimeongezwa kwaajiri ya kusambaza mafaili.
Kwa sasa ni aina moja tu ya mafaili ambayo inaungwa mkono na WhatsApp hii ni aina ya PDF, ni matumaini kwamba matoleo yanayokuja ya WhatsApp yatakuwa yanaunga mkono aina nyingine za mafaili kama vile .doc.
Huu ni mwanzo mzuri kwa WhatsApp kujiimarisha kama app ambayo inatumiwa na watu kwa matumizi zaidi ya kijamii.
One Comment
Comments are closed.