Kuna namna ya kutumia intaneti bila kuhifadhi historia / taarifa, hii ina faida nyingi hasa pale unapotumia kompyuta isiyo ya kwako. Hii ni teknolojia ambayo ipo kwenye kivinjari/Browser kama Google Chrome, Opera n.k
Kwa kawaida wakati unatumia kivinjari/Browser kuingia kwenye mtandao/Internet taarifa zako zote huweza kurekodiwa na kuhifadhiwa hii itakusaidia baadae katika mambo yako kama utahitaji kurudi nyuma ili kujua ulifanya nini. Lakini kuna wakati huhitaji hizi taarifa zibaki kwenye simu yako au kompyuta kwa sababu Mbalimbali. Au unaweza ukawa unatumia simu au kompyuta ya mtu na hauhitaji ajue ulikuwa unafanya nini kwenye kivinjari/browser.

Kuna vipengele au tunaita Features inaitwa New incognito Tab (Private mode). Hii itakusaida kulinda usiri kwenye kifaa kwani ukiwa kwenye hiki kipengele/mode hakuna taarifa yoyote inayohifadhiwa kwenye kifaa chako.
Kama unatumia kivinjari/Browser kama Chrome unatakiwa kwenda kwenye menu bar(:) iliyo mkono wa kulia Juu na utabofya kisha utaweza kuiona na hapo utaichagua na kuifungua.
Mpaka hapo utaweza kufanya mambo yako kwa usiri bila mtu yoyote kujua.
Mda mwingine hatupendi vitu vyetu kuhifadhiwa au kutunzwa kwenye vifaa vyetu pindi tuingiapo kwenye mtandao/internet kwa sababu mbalimbali. Hivyo basi ni bora kutumia hizi teknolojia ambazo zipo kwa ajili ya kutusaidia.
No Comment! Be the first one.