Matumizi ya WhatsApp yanakuwa kila inapoitwa leo na pengine kuna baadhi mtu asipokuwa kwenye muundo huo wa mawasiliano anaonekana “Yupo nyuma” kutokana na ukweli kwamba programu tumishi husika imetokea kupendwa na watu wengi duniani kote.
Kwa wale ambao tunapenda kutumia WhatsApp kupitia vifaa vya kidijiti hakika tunafahamu vyema kuhusu WhatsApp Web lakini ufanyaji kazi wake unategemea kifaa kingine lakini pia uwepo wa intaneti pande zote mbili.
Ni muda sasa kumekuwepo taarifa kuwa kuna maboresho ambayo yanaandaliwa ambapo watu wataweza kutumia WhatsApp katika vifaa tofauti tofauti kwa namba ileile bila shida yoyote. Kwa mujibu wa taarifa za karibu mpango huo upo karibu sana kukamilika na wanaotumia toleo la majaribio basi ndio watakuwa watu wa kwanza kupata huduma hiyo.
WhatsApp kutumika kwenye “Vifaa tofauti tofauti” maana yake nini?
Mara baada ya maboresho hayo kuruhusiwa imaana mtu ataweza kutumia WhatsApp kwenye Android, iOS na hata kompyuta kwa namba yake ileile, bila kutegemea kifaa kingine na kwa mujibu wa habari kwa picha kitu hicho ni kama kipo kwenye majaribio ingawa ni kwa watu wachache sana.

Hayo ndio mambo ya WhatsApp na hatuna budi kukaa tayari kwa kuwa na uwezo wa kutumia programu tumishi husika kwenye vifaa mbalimbali bila ya kutumia namba tofauti tofauti.
Chanzo: Gadgets 360
No Comment! Be the first one.