Kila baada ya muda fulani mfumo endeshi tu bila ridhaa ya yule anaetumia kifaa husika inatunza kumbukumbu za kwenye simu, tabiti, na kuzihifadhi wanapopajua lakini sasa hilo linaenda kubadilika hasa kwenye Android.
Tunapokuwa tumeunganisha vifaa vyetu kwenye intaneti (vinavyotumia Android/iOS) basi tambua tu kwamba kuna wakati mfumo endeshi unaanza tu ktunza vitu kama namba za simu, tarehe muhimu ulizoziainisha kwenye kalenda, n.k kitu ambacho kinachangia katika matumizi ya kifurushi cha intaneti.
Katika maboresho ya hivi karibuni kwenye baadhi ya simu janja mathalani Google Pixel 2 imeonekana Google wameweka kitufe ambacho kinakuruhusu kufanya maamuzi ya kutunza kumbukumbu kwa hiari!.
Kwa vifaa vinavyotumia Android: Kitufe kichakuwezesha kufanya maamuzi ya kutuza kumbukumbu kwa hiari.
Sasisho hilo pia limeonekana kwenye vifaa vinavyotumia Android Marshmallow lakini kiujumla bado hakipo kwa matoleo yote ya programu endeshi husika.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|