Kama ukiangalia katika simu-janja yako au tablet nina uhakika App nyingi ulizoshusha ni za bure, wote tunapenda App za bure. Mara nyingi App za bure zina gharama za faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako. Je unasomaga vigezo na masharti? hapana. Unabonyeza tuu ‘Agree’ katika vigezo na masharti lakini ilibidi usome kwa kuwa waliotengeneza hiyo App wanatoa maelezo kwamba ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao
Watafiti katika chuo cha Carnegie Mellon hivi karibuni wamechambua vigezo na masharti vya App 100 katika google Playstore zinazotumika sana. Walipata App hizi 10 ambazo zinaomba vitu katika simu-janja yako au tableti: Backgrounds HD Wallpaper, Brightest Flashlight, Dictionary.com, Google Maps, Horoscope, Mouse Trap, Pandora, Shazam, Talking Tom Virtual Pet.
Inaingia akilini kwamba App ya Google Maps inaomba kutumia maeneo (locations) kupitia simu yako na App ya kutambua nyimbo Shazam inahitaji kutumia kipaza sauti (microphone) lakini kwa nini App kama virtual pet, dictionary au wallpaper inataka vitu kama hivyo? Mfano Simu za iOs na Android zote zina tochi moja kwa moja huhitaji kushusha App kwa ajili ya hilo
Wakati watafiti wakiangalia App hizo za Android , App zote hizo zina matoleo kwa ajili ya iOs. iOs inakuwezesha kuseti ruhusa (permission) katika kila App. Kama unatumia iOs nenda Settings>>Privacy kuseti ruhusa kwa kila App mfano unaweza ukazima maeneo (location) katika baadhi ya App kama WhatsApp, Facebook n.k.
Ukiachana na iOs, Android haina kuseti ruhusa kwa kila App kama ilivyo iOs. Google walikua nayo kama kipengele kilichojificha (hidden feature) katika toleo 4.4.2 la Android , lakini wakaitoa. Hakuna anaejua lini au kama itarudishwa tena.
Kabla hujashusha App katika Google Playstore kwanza soma App jinsi inavyofanya kazi. Pale wanaomiliki hiyo App wanakua wameacha maelezo kuhusu hiyo App na vitu gani itahitaji
Hizi ni Baadhi ya App zangu nnazozipenda ambazo zina sababu za msingi kwa nini zinataka ruhusa katika baadhi ya vitu katika simu au ziko kifua mbele kwa nini zinahitaji ruhusa hizo
CamScanner – Scan nyaraka zako kutumia kamera ya simu-janja yako
Evernote – App nzuri sana ya kuchukua notisi
Google Translate – Inatafsiri lugha zaidi ya 50
Instapaper – Hifadhi kitu chochote mtandaoni ili usome baadae
JiWire – Tafuta WiFi za bure karibu yako
Kindle – Vinjari na Soma vitabu vya Amazon kimtandao (e-books)
Lumosity – Magemu kuchangamsha akili yako
Magnificent Magnifier HD – Kuwa na Muono wa Karibu kwa kitu chochote
OfferUp – Njia rahisi ya kuuza na kununua vitu kuliko Craigslist
SleepBot – Jua jinsi ya kulala vizuri
Watu wengi walijiuliza kwa nini Facebook Messenger ilihitaji ruhusa kutumia vitu vingi kama camera, audio recording, kupiga namba za simu. Lakini facebook walitoa maelezo mengi sana kwamba kwanini walitaka kila kimoja hapo. Kwa App ambazo zinachukua Data zako katika kifaa chako fanya juu chini na kuwa makini kwamba zinachukua data hizo kwa sababu ambayo ni halali mfano App kama Skype na Google Voice hivi.
Je wewe ni mmoja kati ya wale wanaokubali vigezo na masharti bila kusoma maelezo husika? tuambie sehemu ya comment pia tembelea Instagram, Facebook na Twitter yetu ili usipitwe na makala
No Comment! Be the first one.