Mara kadhaa Apple wamekuwa wakitoa huduma ya kurekebisha simu janja zao BURE na kwa mara nyingine tena bahati imewadondokea walio na iPhone 12 na 12 Pro.
Simu ni kifaa muhimu ambacho kinasaidia katika mawasiliano lakini pia ni kawaida kwa bidhaa hii muhimu kuapata shida na hivyo kuhitaji marekebisho ili kurudi katika ubora/ufanisi wake. Kwa mara nyingine imewalazimu Apple kutoa tangazo la kutengeneza iPhone 12 na 12 Pro ambazo zimebainika kutoa sauti yoyote tuu wakati simu inapigwa.
Zoezi hilo limeanza hivi karibuni na linaonekana likihusisha wateja wenye simu hizo duniani kote ambapo ili kupata huduma hiyo inabidi wazipeleke kwenye duka la bidhaa za Apple linalotambuliwa na kampuni mama.
Je, ni iPhone 12 na 12 Pro zote ndio zinatengenzwa BURE?
Hapana, Apple wameweka wazi kuwa huduma hii itahusisha tu iPhone 12 na 12 Pro ambazo zilitengenzwa kati ya Oktoba 2020 na Aprili 2021. Na kwa kwenda mbali zaidi pengine itawalazimu Apple kuweka angalizo pengine wakabana na kufanya simu hizi zifanyiwe matengenezo kutoka kwenye mkoa/nchi ambayo iPhone 12/12 Pro ilinunuliwa.
Haya sasa wakati ndio huu wa kutumia fursa vizuri lakini tukumbuke kuwa huduma hii ya bure haiwahusu wenye iPhone 12 Mini ama iPhone 12 Pro Max. Haya sasa kazi kwako ewe msomaji wetu kuchukua hatua.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.