Kwa kawaida kabisa makampuni mengi huwa yanaachana na bidhaa Fulani haswa kama bidhaa hiyo ni yenye kuhitaji masasisho ya hapa na pale, Apple wenyewe wameachana kabisa na vifaa kadhaa mwaka 2022.
Apple mpaka sasa wana bidhaa na huduma nyingi sana chini ya mwamvuli wake, kuna baadhi ya bidhaa hizo zipo katika muendelezo wa kuzalishwa na kuna zingine wameachana nazo kabisa.
Leo TeknoKona inakuletea huduma hizo
iPod touch
Hii tulikundikia >>HAPA<< na ni kwamba bidhaa hii Apple waliachana kabisa na uzalishaji wake wala hakutakua na toleo lingine lolote la huduma hii.
Ikumbukwe vizuri kwamba iPod ndio ilisababisha mpaka iPhone ikaanza kutengenezwa na ilikuja kwa kuzingatia kwa kiasi kikubwa muonekano wa iPod
iPod ziko katika matoleo kadha wa kadha lakini kwa mwaka 2022 Apple wenyewe walitangaza kwamba wanaachana kabisa na uzalisha wa bidhaa hizo. iPod ya kwanza kabisa ilitoka mwaka 2001.
iMac Ya Inchi 27
licha ya ufanyaji wake vizuri katika soko, iMac za mfumo huu hazitakua zinazalishwa tena, kumbuka mwezi machi Apple walitambulisha Mac Studio na Studio Display. iMac hiyo ambayo haitengenezwi tena ni ile ambayo ilikua inatumia prosesa kutoka kampuni ya Intel.
Muendelezo Wa Matoleo Ya Zamani Ya Apple Watch.
Tokea Apple watch kuanzishwa mpaka sasa ni wazi kabisa kwamba imebadilika kutoka kwenye muonekano hadi kwenye ufanyaji (ufanisi) wake wa kazi.
Kwa sasa kuna toleo la Apple Watch Ultra ambalo linakuja likiwa na jumba la titani (titanium), hili ndio linakua toleo jipya katika soko maana Apple wanaachana na matoleo ya mendelezo wa zaman yaani Apple Watch Series (mfano Apple Watch Series 8)
Apple TV HD
Apple TV zimetoka katika muundo mpya hivyo basi hata Apple wenyewe wameona waachane kabisa na Apple TV HD maana kwa sasa kuna Apple TV 4K ambazo zimetoka mwezi oktoba.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi kuna kifaa kingine kutoka Apple ambacho nimekisahau?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.