Kuna teknolojia nyingi sana ambazo zilizinduliwa na zikawaacha watu wakibaki midomo wazi, Google Glass ni moja katika ya teknolojia hizo kutoka kampuni ya Google.
Sio mara ya kwanza kampuni kuanzisha bidhaa au biashara na kisha kufa, hivyo basi sio mbaya sana hata kwa Google Glass.
Kumbuka iliundwa kampuni kabisa ambayo iko chini ya Google ambayo imekua ikiwa inahusika na maswala ya kutengeneza miwani hii toka mwaka 2013.
Miwani hii kwa kiasi kikubwa ilikua inahusishwa na teknolojia ya uhalisia wa bandia yaani augmented reality na baada ya toleo la miwani hizo kutoka hazikufanya vizuri katika soko.
Ni wazi kwamba kwa wakati ule kampuni ya Google iliwahi sana katika kuingia katika aina hii ya teknolojia maana kwa hivi karibuni ndio makampuni mengi makubwa yameonekana yakikimbilia huko.
We're gearing up for #GoogleIO and we want to know – what excites you most about the future of AR? Sound off in the replies! ↓
— Google AR & VR (@GoogleARVR) March 11, 2023
Sasa basi kilichowashangaza wengi ni kwamba mwanzoni kabisa mwa wiki hii kampuni ilitangaza kabisa kwamba kampuni hiyo inafunga kabisa uzalishaji wa miwani hizo.
Kutoka katika tovuti ya Google Glass wao wenyewe wametoa taarifa ya kwamba wao wataendelea kutoa msaada wa kitaalamu kwa miwani ambazo tayari zipo kwa wateja lakini msaada huo una kikomo.
Mpaka kufikia septemba 15 ya mwaka huu utakua ndio mwisho wa msaada wa kitaalam (support) kwa watumiaji wote wa miwani hiyo yaani hapa hata huduma ya vipuri haitapatikana tena.
Wateja wengi wameshtushwa na jambo hili kutoka kwao Google Glass maana wengi wanadaida angalau wangepewa maelezo ya kutosha kuhusiana na hili ukiachana na sababu ya kampuni kufanya vibaya katika soko
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la maoni je unadhani ni sawa kuanzisha bidhaa na baada ya muda kuachana kabisa kuzalisha biashara hiyo na pia kutotoa tamko la kueleweka kwa wateja wako?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.