Tumeshawahi kundika mengi sana kuhusiana na mtandao wa Spotify, pitia kidogo hapa. lakini hivi unajua kuhusu Spotify Stations?
Spotify Stations ni huduma ya redio kutoka katika mtandoa wa muziki wa Spotify. Huduma hiyo ina App tofauti kabisa na App ya spotify ile ya kawaida ile tuliyoizoea.
App hii ilikua mahususi kwa ajili ya vipindi vya redio na ilizalishwa mwaka 2018 na kwa sasa mtandao huo umeamua kuachana kabisa na huduma hiyo.
Kinachofanyika hapa ni kwamba inafungia huduma zote za ki’App na zile za kimtandao kabisa, mpaka kufikia mwezi wa 5 tarehe 16,2022.
This sucks! pic.twitter.com/QaQrNBdHBP
— Jared Newman (@OneJaredNewman) May 5, 2022
Mpaka sasa bado kampuni haijaweka wazi sababu za kuachana na App hiyo, lakini imesema inarudisha stesheni za redio katika App ya Spotify amabyo imezoeleka ili watu waendelee kusikiliza.
Hapa kinachofanyika ni kwamba, mtandaoni huduma hii haitapatikana, App yake haipatikani tena katika soko la App la Playstore, lakini kama bado una App katika simu unaweza ukaitumia pengine mpaka tarehe 16.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niambie Hapo Chini Katika Uwanja Wa Comment, Taarifa Hii Umeipokea Vipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.