Mtandao wa Twitter umefanya mambo mengi sana katika jitihada zake za kuzifanya hisa zake ziweze kupanda bei sokoni, lakini kinyume na jitihada za mtandao huu hisa zake sokoni zimekuwa zikiporomoka kila uchao mfano wa gari bovu katika mteremko mwanana.
Tangu siku ya kwanza ambapo Twitter iliandikishwa katika soko la hisa nchini marekani hisa zake zimekuwa zikishuka na kushuka kitu ambacho kwa tafakari ya haraka ni kwamba wawekezaji wanaona kwamba biashara hii haina faida lakini kwa jicho la mbali hii inamaana kwamba pengine mtandao huu hautakuwepo miaka mingi baadae.
Pengine unawaza ni kwanini Twitter wanashindwa kufanya vizuri katika soko kama ilivyo kwa mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, katika makala hii nitajaribu kuonesha baadhi ya sababu ambazo zimepelekea mtandao huu kuwa hapa ulipo sasa pia nitajadili yale ambayo Twitter imefanya kujaribu kunusuru bei za hisa zake.
Twitter ni mtandao mgumu kutumia
Tofauti na mitandao kama Facebook ambayo ni rafiki na watumiaji ni rahisi kuwa mwenyeji haraka, Twitter imekuwa ni ngumu kidogo kwa watumiaji wapya. Sio kitu kigumu kukutana na mtu akakwambia kwamba alishindwa kuuelewa mtandao huu unavyofanya kazi.
Kimsingi hii ndiyo sababu kuu ya kushindwa kwa mtandao huu katika soko, inachangia kwa Twitter kuwa na watumiaji walio hai wachache ambao wanaongezeka kila siku hii inasababisha isiwe inapata matangazo ya kutosha (ambayo yangeleta mapato makubwa) na hivyo thamani ya hisa zake kushuka.
Twitter ni jeshi la mtu mmoja
Ndio Twitter inategemea watumiaji wa App yake kuu tu kwa ajiri ya kutengeneza wigo wa matangazo ya mtandaoni ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mapato kinachokuza thamani ya hisa, wakati mtandao kama Facebook unakusanya watumiaji kutoka Facebook na pia kutoka katika app yake ya Instagram ambayo inafanya vizuri katika mitandao ya kijamii. Facebook imefanikiwa kumiliki apps nyingine kubwa zinazofanya vizuri na hivyo kuzidi kuipa hadhi zaidi.
Twitter wamekuwa wanachelewa kufanya maamuzi ya muhimu.
Mtandao huu umekuwa ukichelewa kufanya maamuzi ama mabadiliko ya maana kila wakati yanapohitajika na hii imekuwa ikiigharimu kampuni hii kibiashara. Kwanza ni kuchelewa kubadilisha mfumo wa uendeshaji wake wakati ilipoanza ili kuweza kutengeneza mapato makubwa zaidi ( Twitter ilipoanza ilikuwa katika muundo ambao haukuwa umekaa kiukusanyaji wa mapato zaidi).
Pili Twitter walichelewa kumuweka Jack Dorsey katika nafasi ya Utendanji mkuu baada ya hatua za kumtoa Dick Costolo kufanikiwa ili Jack Dorsey aingie katika nafasi hiyo na kufanya mabadiliko ambayo yalikuwa yakihitajika.
2 Comments
Comments are closed.