Lenovo ni moja kati ya kampuni la kiteknolojia linalofanya vizuri sana katika soko, kampuni hili linajulikana sana kwa ubora wake katika soko la simu janja na kompyuta.
Lenovo wao kwa sasa kuna aina za simu ambazo wao wamezipiga chini hali ya kwamba imewashangaza wengi.
Simu hizo si zingine bali ni zile ambazo walizalisha na kuziuza mahususi kabisa kwa aji ya watu kucheza magemu mbalimbali kupitia kifaa hicho.
Simu hizo zilikua zimepewa jina la “Legion Mobile Gaming Phones’ na lengo lake kubwa ilikua ni kujitenga na simu janja za kawaida katika kampuni hiyo na kuhakikisha bidhaa hii inajitegemea.
Kilichowashtua wengi ni kwamba Lenovo wenyewe walitangaza kuwa kwa sasa wanaachana kabisa na biashara hiyo, ina maana kwa haraka haraka ni kwamba hakutakua na simu inayozalishwa kutoka katika kundi hili.
Kingine cha kukiweka akilini ni kwamba kampuni hiyo haijatangazwa kwamba inaacha kabisa kujihusisha na maswala ya magemu… kumbuka saa nyingine maamuzi kama haya ndio huwa yanapelekea kampuni kuja na njia nzuri zaidi (labda ya kufurahia magemu).
Kumbuka simu janja ambazo zipo mahususi kwa ajili ya magemu zipo nyingi tuu hivyo Lenovo hakuwa peke yake katika soko.. kuna kampuni kama ASUS, Xiomi, Nubia Red Magic na nyingine nyingi zilikua na vifaa vya aina hii katika soko.
Lakini mpaka sasa haijulikani kwa zile simu ambazo zipo katika soko –au kwa watu— kwamba zitaathirika na uamuzi au hapana —pengine tusubirie tamko kutoka kwao Lenovo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, unadhani Lenovo pengine wanataka kuja na kifaa kingine cha kucheza gemu kama vile Playstation?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.