Teknolojia ya ‘fingerprint sensor’ inaboreshwa zaidi kutokana na ujio wa teknolojia mpya ya uwekaji wa senza hizo kutoka LG.
LG wametengeneza teknolojia mpya ya uwekaji wa sensa za fingerprint kupitia vioo (display) za simu badala ya teknolojia ya sasa ambapo inaitajika kuwe na sehemu spesheli ya kugususa kidole – mfano kwenye iPhone ni kwenye kitufe cha Home, wakati simu zingine kama vile Tecno zenye sensa hizo sehemu inakuwa ni nyuma ya simu.
Kimombo teknolojia za kisasa za ‘fingerprint sensors’ zinafahamika kama ‘button type fingerprint’, teknolojia ya LG inaleta ‘buttonless fingerprint sensors’
Kutokana na uondoaji huu wa eneo jingine la kuweka sensa hizo inamaanisha kutaokoa nafasi zaidi kwenye simu na pia kutasaidia utengenezaji wa simu nyembamba zenye teknolojia ya ‘fingerprint sensor’.
Kwa teknolojia ya LG kuunlock simu yako kutaitaji wewe kuweka kidole chako juu ya kioo cha simu yako tuu. Baada ya majaribio mbalimbali inaonekana nafasi ya sensa hizo kufanya makosa ya kukubali alama ya kidole cha mtu mwingine ni ndogo sana, nayo ni uwezekano wa takribani asilimia 0.002 tuu.