Kampuni la LG kutoka korea, limetengeneza keyboard ndogo ambayo inaweza kutumika kwenye vifaa kama vile kompyuta n.k. Keyboard hii ni ndogo sana kwa umbo na la kuvutia zaidi ni kwamba inakunjika
Keyboard hii imepewa jina la ‘Rolly Keyboard 2’ na kampuni inawahakikishia watumiaji kuwa na urahisi wakati wanaitumia katika kufanya kazi zao mbali mbali kama vile kuandika vitu.
Mara ya kwanza LG walitoa Keyboard ya chini yake ambayo waliipa jina la ‘LG Rolly’ na sasa wamekuja na toleo la pili la keyboard hiyo.
Cha kuvutia kingine katika keyboard hiyo ni kwamba ina mistari mitano tuu ya vibonyezo. Uchache wa mistari hiyo ya vibonyezo unaiwezesha Keyboard hii kujipatia umbo dogo kabisa.
Mambo mapya katika keyboard hii ni kibonyezo cha TAB ambacho kimewekwa kwa upande wa chini mwishoni mwa vibonyezo vingine. Pia LG wameboresha katika uwezo wa huduma ya Bluetooth katika kifaa hiki.
Kifaa hiki kinakuja na betri lile la mfumo wa 1 AAA. Kwa sasa keyboard hii ambayo inatumia mfumo wa QWERTY inapatikana kwa wateja ambao wapo korea. LG hawataishia hapa kwani keyboard hii ni ya aina yake kwa hiyo wana mipango mikubwa ya kuongeza soko lao kwa kuvuka mipaka.
Kingine cha kuvutia zaidi kuhusiana na keyboard hizi ni kwamba zinaweza zikatumika katika simu za iOS, Android na Windows