Li-Fi ni teknolojia itumiayo miale ya mwanga kusafirisha data(visible light proton). Teknolojia hii ya mawasilano husafirisha data katika spidi ya juu mara 100 zaidi kulinganisha na teknolojia ya Wi-Fi itumiayo mawimbi ya redio(radio waves).
Teknoljia hii itamuhitaji mtumiaji kuwa na kifaa maalumu cha kupokea mwanga ( led bulb),kifaa cha kutambua mwanga na Munganisho intaneti kutumia teknolojia hii.
Uvumbuzi huu wa kihistoria ulifanywa na Prof Harald Haas ambaye sasa ni mkurungezi mtendaji wa kampuni ya PURELIFI inayoshughulika na utoaji wa huduma za mfumo huu wa mawasilano. Uvumbuzi huu umejaribiwa na kuthibitika kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu. Teknolojia hii hutumika katika vifaa vyote viwezavyo kuunganishwa na intaneti kama Simu, Kompyuta, Tv na vingine.
Prof Haas aliushutua ulimwengu wa teknolojia pale alipoitambulisha teknolojia hii ambayo sasa lifi inaweza kusafirisha data mpaka kwa spidi ya GB Moja kwa sekunde 1GbPs lakini inasemekana kuweza kufikia 224GbPs. Yaani itakuwezesha kudownload muvi yenye ukubwa wa Gb 1 kwa sekunde moja tu.
Faida kubwa za utumiaji wa teknolojia hii ni kwamba kwanza amna muingiliano wa signal hivyo itakuwa na manufaa makubwa kama itatumika katika sehemu ambazo mwingiliano wa signals ni tatizo kama katika ndege. na pili kutakuwa na usalama kwa mtumiaji zidi ya udukuzi kwani miale hii haiwezi kupitiliza katika ukuta
Ingawaje teknolojia hii haitafanya kazi pale kifaa kitoacho mwanga led bulb kitakapozimwa hivyo bhasi bhasi itamulazimu mtumiaji kuwasha taa muda wote. Uzuri ni kwamba taa zitakazo tumika katika lifi zimetengenezwa kwa mfumo wa hali ya kiasi cha kwamba inaweza kuwaka bila kutoa mwanga uonekanao.
No Comment! Be the first one.