Watu wengi wanaweza wasiwe na akaunti Linkedin lakini ni mtandao wa kijamii ambao “Hauna mabo mengi” na makampuni mengi duniani yanatumia akaunti zao kwa ajili ya kutangaza ajira, kuwasiliana na watu, n.k.
Linkedin ambayo kwa sasa ipo chini ya Microsoft baada ya kununuliwa miaka kadhaa iliyopita imekuwa ikiaminika na watu wengi duniani kutokana na misingi iliyojiwekea na hata waajiri kutoka mataifa mbalimbali wakitangaza kazi wakati wa kujaza fomu ya maombi ya wengi wanaweka sehemu ya mtu kuweka kiunganishi cha akaunti yake Linkedin ambapo wataweza kufahamu mengi ya muhimu kuhusu mhusika anayeomba kazi.
Takribani mwaka mmoja tangu Linkedin wapeleke kipengele cha Stories ndani mtandao huo wa kijamii wakati wake wanaonekana kufikia tamati kwani kuanzia Septemba 30 hakitakuwepo na badala yake wahusika wanasema wanafanya maboresho na kuja kipengele kipya cha kupandisha video (picha mnato/jongefu) fupifupi za kati ya sekunde 10-30.
Wapo wale ambao wana matangazo yao waliyoyalipia na tayari yapo hewani kwenye Linkedin Stories na kimsingi hatua hii ya kukifunga wataathiriwa na hatua hivyo. Hivyo, watu ambao tayari walishalipia huduma ya matangazo kwa ajili ya kuonekana kwenye Stories yatakuwa yakionyeshwa kwenye ukurasa wa mbele (feed). Halikadhalika, kwa wale ambao wamelipia matangazo moja kwa moja kutoka kwenye Stories itawalazimu kuyatengeneza upya.

Kila chenye mwanzo kina mwisho wake na ni baada ya mwaka mmoja tu Linkedin wanaamua kuachana na kipengele cha Stories lakini kufungwa kwa mlango mmoja kunafungua njia ujio wa picha jongefu fupifupi ndani mtandao wa kijamii husika.
Vyanzo: TechCrunch, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.