Kama unapenda kupicha picha Luminance HDR ni kwa ajili yako. Hivi ulishawahi kupiga picha ambayo mwanga ukawa mdogo sana au ukawa mwingi sana?
Kwa mfano hata ukipiga picha mbele ya jua unaweza ukashangaa katika picha linatokea jua (kali) na mtu katika hali ya weusi ulipitiliza (kiasi cha kwamba unaweza usione sura ya mtu vizuri), na mara nyingine unaweza ukaona rangi ya nguo tuu.
Luminance HDR inaweza ikasaidia kwa kiasi kikubwa. Ukichukua picha hiyo hiyo uliyoipiga (ambayo jua linaonekana sana, na mtu anaonekana nguo) unaweza ukaibadilisha na kuwa picha ya kawaida ambayo mtu wa kawaida anaweza akaona kila kitu katika picha hiyo.
Luminance HDR pia inaweza ikatengeneza mafaili mengi ya HDR kutoka katika picha moja. Licha ya hivyo pia inaruhusu kubadilisha rangi, kuizungusha, kuibadilisha saizi na ukishamaliza kuifanyia hayo yote unaweza ukaisevu
Programu hii pia inasapoti mafaili katika mfumo wa HDR na LDR.
Shusha Windows – Bure
Shusha Mac – Bure
Mpaka hapo kama una picha ambazo mwangaza wake haupo kawaida – yaani ni mwingi sana au mdogo sana – Programu (Luminance HDR) hii itakuwa ndio mkombozi wako.Kizuri ni kwamba inapatikana bure na pia kama programu nyingi za bure zilivyo wakati wa kuipakua itakuomba kuchangia (lakini unaweza kukataa na kuendelea kupakua).